Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, October 6, 2016

JESHI STARS YAPOKEA KIPIGO CHA TANO TOKA KWA KPA YA KENYA

TIMU ya Jeshi Stars jana imepokea kipigo cha tano mfufulizo baada ya kufungwa na KPA ya Kenya vikapu 73 kwa 41 kwenye mashindano ya kanda ya tano uliochezwa Uwanja wa Ndani wa Taifa.
Awali mchezo huo ulichelewa kuanza kwa sababu Jeshi Stars walikuwa wakidaiwa ada ya ushiriki hivyo kuzuiwa kucheza hadi walipe pesa iliyokuwa imesalia.
Baada ya muda walilipa kiasi cha dola 180 kwani walitakiwa kulipa dola 20 kwa kila mchezaji.
Akizungumza na gazeti hili kocha wa Jeshi Stars, Peter Samson alisema timu yake imekuwa ikifanya vibaya kutokana na maandalizi hafifu waliyokuwa nayo kwani walianza mazoezi wiki mbili kabla ya kuanza kwa mazoezi.
“Sisi tulipata barua ya kushiriki mwishoni mwa Septemba hivyo muda wa mazoezi ulikuwa wiki mbili muda ambao ni mchache kuandaa timu”, alisema Samson.
Jeshi Stars juzi ilifungwa na UCU vikapu 73 kwa 35, ikafungwa na USIU , UBUMWE, KCCA na leo itacheza na Donbosco ya Tanzania kwenye mchezo wa kukamilisha ratiba.