Mkurugenzi Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba akizungumza na wandishi wakati wa kumtambulisha Abdul Mohamed ambaye ni Meneja mkuu wa Azam FC |
UONGOZI wa Azam
FC, umesema umeshatuma uhamisho wa kimataifa (ITC) wa Farid Mussa nchini
Hispania lakini kibali cha kufanya kazi ndio kinamkwamisha kuondoka nchini.
Akizungumza
na wandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba alisema
Azam wameshawatumia hati ya uhamisho ya kimataifa (ITC) kwa klabu ya Tenerrife
inayoshiriki ligi daraja la kwanza ambayo imekuwa ikihitaji huduma za winga
huyo
“Suala la
Farid lipo kwenye hatua nzuri muda si mrefu winga huyo ataelekea nchini
Hispania kwakua kila kitu kinaenda sawa, tunasubiri kibali cha kazi
kikipatikana hata kesho anasafiri,"
Pia Kawemba
alisema hawezi kumkwamisha Farid kucheza soka la kulipwa kwa sababu wamempeleka
kwa mkopo na ndio wanagharamia kila kitu kwa makubaliano ambayo wamewekeana na
klabu ya Tenerrife kuwa watakuwa wanapeleka wachezaji na wao watakuwa
wanawaleta wachezaji Azam FC.
Kawemba
alitolea ufafanuzi swala la timu yao kuvaa nembo ya mdhamini wa ligi kuu
Tanzania bara kwenye mkono mmoja na kudai wakati wanatisha kanuni ilisemekana
timu ikipata mdhamini itumie mkono huo mwingine hivyo na wao wamepata mdhamini
mwingine.
“Kwanza
sijapata barua kuwa tumepigwa faini na shirikisho la soka Tanzania (TFF) na
endapo tutapata tutaeleza sababu ya sisi kutovaa maana lakini kwenye viwanja
kuna matangazo ya wadhamini ambayo klabu hazina taarifa zake”, alisema Kawemba.
Kawemba
alifika mbali na kusema hiyo kanuni ya kuvaa nembo ya mdhamini kwenye mikono
yote iondolewe kama ilivyoondolewa kanuni ya mchezaji mwenye kadi nyekundu
kuchagua mchezo wa kucheza.
Wakati huo
huo, Kawemba amemtambulisha Abdul Mohamed kuwa Meneja Mkuu wa Azam FC, ajira
ambayo ameanza kuitumikia kuanzia Septemba.
Kawemba
alisema wamemchukua Mohamed ili kuboresha klabu yao kwenye ushindani wa
uwanjani na nje ya uwanja kwani soka kwa sasa ni biashara kubwa duniani.
Naye Mohamed
ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na mtaalamu wa Fedha, Uhasibu na Uchumi
alisema amefurahi kuwa familia ya Azam na kuomba ushirikiano ili kufanikisha
majukumu ya kila siku.
No comments:
Post a Comment