Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji Jumapili ya Septemba
4, 2016 inatarajiwa kutoa hukumu ya shauri la mchezaji Hassan Ramadhan
Kessy anayedaiwa na Klabu ya Simba kuvunja mkataba kwa kuanza kufanya
mazoezi na klabu ya Young Africans sambamba na kusajili katika timu hiyo
ya Mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam kabla ya mkataba wake kufika mwisho
Juni 15, 2016.
Simba imelalamika mbele ya kamati hiyo ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kuwa, mchezaji Hassan Kessy alivunja taratibu hizo
akiwa ndani ya mkataba wa klabu hiyo yenye mashakani yake Barabara ya
Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati hiyo, shauri hilo lilisikilizwa na
uamuzi wake utatolewa Jumapili ijayo. Hii ni baada ya kushindikana
kusikilizwa kwa shauri jingine linalohusu Klabu Simba ikiilalamikia
Klabu Young Africans, kuingia mkataba na mchezaji Hassan Ramadhani Kessy
wakati bado ana mkataba na klabu Simba.
Shauri la Simba dhidi ya Young Africans lilishindika kusikilizwa kwa
sababu Young Africans hawakutokea mbele ya kamati hiyo wakati wa
kusikiliza shauri hilo, hivyo kamati itaiandikia barua Young Africans
kukumbushwa kuhudhuria kwenye kesi hiyo Jumapili ijayo kabla ya kutolewa
uamuzi. Kama hawakutokea tena, shauri hilo litasikilizwa upande mmoja
na kutolewa uamuzi upande mmoja.
Katika mashauri mengine,
Mathias Lule v Stand United
Malalamiko ya Kocha Mathias Lule. Lule anadai
mshahara, usajili na bima ya matibabu kwa Stand United. Kamati imeridhia
pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo
wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
Ametre Richard v Simba
Madai ya malimbikizo ya mishahara kwa Ametre
Richard dhidi ya Simba. Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza
suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamekubaliana kukutana
Jumatano Agosti 31, 2016 na kuleta yatokanayo TFF.
Wachezaji watatu v Mbeya City
Kamati umeamua kuwa Mbeya City ya Mbeya iwalipe
wachezaji wake wa zamani, Abdallah Juma, Temi Felix na Erick Mawala
madai yote ya malimbikizo ya mshahara na fedha za usajili.
Kinondoni Sports Academy (KISA) v klabu 5 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
(i) KISA
inadai fidia za malezi kwa Azam baada ya kumsajili mchezaji Omary
Maunda, ambako Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo
nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo
na na kuleta yatokanayo TFF.
(ii) KISA inadai
fidia za malezi kwa Kagera Sugar baada ya kumsajili mchezaji Hussein
Abdallah, ambako Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala
hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya
hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
(iii) KISA inadai
fidia za malezi kwa Mtibwa Sugar baada ya kumsajili mchezaji Daniel
Jemedari, ambako Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala
hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya
hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
(iv) KISA inadai
fidia za malezi kwa Majimaji ya Songea baada ya kumsajili mchezaji
Joseph Njovu. Shauri hili sasa litasikilizwa Jumapili ijayo ya Septemba
4, 2016 baada ya kushindikana kusikilizwa kutokana na mdaiwa Majimaji
kutotokea kwenye kesi. Majimaji wameagizwa kukuhudhuria shauri hilo
vinginevyo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja.
(v) KISA inadai
fidia za malezi kwa Toto African ya Mwanza baada ya kumsajili mchezaji
Jafari M. Jafari, ambako Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza
suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja
kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
(vi) KISA inadai
fidia za malezi kwa JKT Ruvu ya Pwani baada ya kumsajili mchezaji Najimu
Maguru, ambako Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala
hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya
hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
SPUTANZA v Young Africans
Chama cha Wachezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania
(SPUTANZA), kilileta malalamiko dhidi ya Young Africans kuhusu madai ya
usajili wa Jerry Tegete, Omega Seme na Hamisi Thabiti. Shauri hili sasa
litasikilizwa Jumapili ijayo ya Septemba 4, 2016 baada ya kushindikana
kusikilizwa kutokana na mdaiwa Young Africans kutotokea kwenye kesi.
Young Africans wameagizwa kukuhudhuria shauri hilo vinginevyo
litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja.
Coastal Union v Simba SC
Coastal Union ilileta malalamiko dhidi ya Simba
Sports Club kuhusu madai ya fidia ya wachezaji Ibrahim Shekwe, Hemed
Hamisi na Abdi Banda. Imeamuriwa kuwa Simba iilipe mara moja Coastal
Union fidia ya shilingi milioni tano.
Coastal Union v Kagera Sugar
Coastal Union ilileta malalamiko dhidi ya Kagera
Sugar kuhusu madai ya fidia ya mchezaji Ibrahim Sheku. Kamati imeridhia
pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo
wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
Coastal Union v Mbeya City
Coastal Union ilileta malalamiko dhidi ya Mbeya
City kuhusu madai ya fidia ya wachezaji Fikirini Bakari na Ayub Yahaya.
Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati
kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta
yatokanayo TFF.
Coastal Union v Young Africans
Coastal Union ilileta malalamiko dhidi ya Young
Africans kuhusu madai ya fidia ya mchezaji Juma Mahadhi. Shauri hili
sasa litasikilizwa Jumapili ijayo ya Septemba 4, 2016 baada ya
kushindikana kusikilizwa kutokana na mdaiwa Young Africans kutotokea
kwenye kesi. Young Africans wameagizwa vinginevyo kukuhudhuria shauri
hilo litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja.
Coastal Union v JKT Ruvu
Coastal Union ilileta malalamiko dhidi ya JKT Ruvu
kuhusu madai ya fidia ya mchezaji Yusuf Chuma. Shauri hili sasa
litasikilizwa Jumapili ijayo ya Septemba 4, 2016 baada ya kushindikana
kusikilizwa kutokana na mdaiwa JKT Ruvu kutotokea kwenye kesi. JKT Ruvu
wameagizwa kukuhudhuria shauri hilo vinginevyo litasikilizwa upande
mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja.
Bakari Shime v Mgambo JKT
Malalamiko ya Kocha Bakari Shime kudai ya mshahara
dhidi ya Mgambo JKT. Kamati umeamua kuwa Mgambo JKT imlipe Shime na
uongozi wa klabu hiyo umeahidi kumlipa Shime kiasi cha Sh 8,500,000
ndani ya wiki tatu kuanzia tarehe ya uamuzi huu.
Mchezaji Ally Rashid Ally v Simba
Malalamiko ya Mchezaji Ally Rashid Ally kudai
kunyimwa stahiki zake na Klabu ya Simba. Shauri hili sasa litasikilizwa
Jumapili ijayo ya Septemba 4, 2016 baada ya kushindikana kusikilizwa
kutokana na mdai Ally Rashid Ally kutotokea kwenye kesi. Ally Rashid
Ally ameagizwa kukuhudhuria shauri hilo, vinginevyo litasikilizwa upande
mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja.
Wachezaji Omary Seseme, Said Omary na Edward Christopher v Toto African
Malalamiko ya wachezaji Wachezaji Omary Seseme,
Said Omary na Edward Christopher dhidi ya Toto African kudai mishahara
na fedha za usajili. Kamati umeamua kuwa Toto African iwalipe wachezaji
hao na uongozi wa klabu hiyo umeahidi kumlipa ndani ya wiki mbili
kuanzia tarehe ya uamuzi huu.
Wachezaji Rajab Isihaka na Said Mketo v Ndanda FC
Malalamiko ya wachezaji Rajab Isihaka na Said
Mketo v Ndanda FC dhidi ya Ndanda kudai mishahara na fedha za usajili.
Kamati imeridhia pande mbili kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati
kama ambavyo wameomba. Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta
yatokanayo TFF.
Simba SC v Mbaraka Mussa Yusufu
Simba ilileta malalamiko dhidi ya Mchezaji Mbaraka
Mussa Yusufu kuhusu madai ya utoro kazini. Kamati imeridhia pande mbili
kwenda kulimaliza suala hilo nje ya kamati kama ambavyo wameomba.
Wamepewa wiki moja kufanya hivyo na na kuleta yatokanayo TFF.
Lipuli FC v Mbeya City
Lipuli ilileta malalamiko dhidi ya Mbeya City
kumsajili mchezaji Mackyada Makolo bila kufuata utaratibu. Shauri hili
sasa litasikilizwa Jumapili ijayo ya Septemba 4, 2016 baada ya
kushindikana kusikilizwa kutokana na mdaiwa Mbeya City kutotokea kwenye
kesi. Mbeya City wameagizwa kukuhudhuria shauri hilo vinginevyo
litasikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi upande mmoja.
Lipuli v Ruvu JKT
Lipuli ilileta malalamiko dhidi ya JKT Ruvu
kumsajili Mchezaji Kassim Kisengo bila kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja
na kutolipa ada ya mkoa na wilaya. Pande zote mbili zilimalizana.
No comments:
Post a Comment