Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 12, 2016

VAN GAAL ASEMA KUSHAMBULIWA BASI SI KISINGIZIO CHA KUFUNGWA NA WEST HAM

MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal amekataa kusingizia kushambuliwa kwa Basi la Timu yao nje ya Uwanja wa Upton Park Jana Usiku ndiko kulisababisha Timu yake kufungwa 3-2 na West Ham na kuhatarisha wao kuikosa 4 Bora ya BPL, Ligi Kuu England.
Wakielekea Uwanjani kabla ya Mechi hiyo ya kihistoria kwani ndio ilikuwa ya mwisho kabisa kwa West Ham kuchezea Uwanja wa Nyumbani Upton Park, Basi la Timu ya Man United lilipigwa Chupa na Makopo na kuvunjwa Vioo kadhaa.
Baada ya kipigo chao, Van Gaal alisema kulaumu kushambuliwa Basi lao ni kutafuta kisingizio lakini alikiri hilo pengine limeathiri Wachezaji wake chipukizi.
Van Gaal, mwenye Miaka 64, alisema: “Nina uzoefu mkubwa kwenye Soka na wapo Wachezaji hawana uzoefu huo.”
Hata hivyo, Van Gaal anaamini bado wana nafasi ya kufuzu 4 Bora wakiwafunga Bournemouth Jumapili Uwanjani Old Trafford kwani Wapinzani wao Man City wana Mechi ngumu ya Ugenini na Swansea City.