Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 23, 2016

VAN GAAL ACHUNGULIA MLANGO WA KUONDOKEA, JOSE MOURINHO KUITHI MIKOBA YAKE

WAKATI WAKALA wa Jose Mourinho, Jorge Mendes, maarufu kama 'Supa Wakala' akitua London, Meneja wa Manchester United Louis van Gaal tayari amewaaga Wasaidizi wake na Wafanyakazi wengine.
Jumamosi Man United walitwaa FA CUP huko Wembley Jijini London walipoifunga Crystal Palace likiwa Taji lao la kwanza kubwa tangu Sir Alex Ferguson astaafu Mwaka 2013, Jana Van Gaal akiondoka Hoteli waliyofikia huko London aliwaambia Maripota kuwa 'Imekwisha!'.
Baadhi ya Wachambuzi walidai kuwa kauli hiyo ina maana kuwa himaya yake huko Old Trafford imekwisha lakini Man United imesema alimaanisha Msimu umekwisha.
Lakini habari za ndani zimedai Van Gaal amewaaga Wafanyakazi wenzake huku akiwaambia hana hakika kama wataonana Msimu ujao.

Van Gaal amebakiza Mwaka Mmoja katika Mkataba wake wa Miaka Mitatu na Man United.
Kufika kwa Jorge Mendes huko London akitoka Shanghai, China kunasemekana kuwa ni kwa ajili ya Mkutano wa Jumanne ambao yeye, Mourinho na Makamu Mwenyekiti wa Man United Ed Woodward watahudhuria ili kukamilisha Mkataba wa Mourinho huku uthibitisho wake kuwa Meneja mpya wa Man United ukitolewa mara tu baadae.
Mourinho, Raia wa Ureno mwenye Miaka 53, amekuwa hana kibarua tangu aondoke Chelsea Mwezi Desemba ikiwa ni Miezi 7 tu tangu aipe Ubingwa wa England ukiwa ni Ubingwa wa 3 katika himaya zake 2 hapo Chelsea.