Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 9, 2016

RUVU SHOOTING YAINGIA KAMBINI KUJINOA NA LIGI KUU
TIMU ya Ruvu Shooting imeingia kambini jana kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2016/17 utakaoanza mwezi Agosti.
Akizungumza na gazeti hili msemaji wa timu hiyo Masau Bwire, alisema timu itaweka kambi ya mazoezi katika eneo la 832 Ruvu JKT, Uwanja wa Mabatini chini ya Kocha Mkuu, Tom Olaba akisaidiwa na Seleman Mtungwe.

“Wachezaji waliripoti kambini juzi baada ya mapumziko mafupi waliyopewa baada ya kumalizika kwa Ligi Daraja la Kwanza (FDL)  na tutafanya usajili kujaza nafasi za kipa, namba 2, 4, 6, 8, 9 na 10”, alisema Masau.

Pia Masau alisema lengo la kufanya usajili na kuanza kambi ya mazoezi mapema, ni kukiimarisha kikosi chao ili kiwe cha ushindani zaidi, msimu ujao wa ligi waweze kutwaa ubingwa wa soka Tanzania Bara.

Masau alisema wanataka kuja sawa  kwenye ligi kama  Leicester City ya England ilivyofanya kwenye ligi yao.
“Tuna imani kuyafikia malengo yetu kwani, tunayo dhamira ya dhati kabisa, ndio maana tunaanza kambi mapema. Ombi letu ni HAKI ifanyike kwa kila eneo wakati wote wa ligi, tunaweza, tutakuwa mabingwa kwa uwezo wa kucheza mpira” alimalizia Masau