Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, January 6, 2016

SIMBA KUCHEZA NA BURKINAFASO KOMBE LA SHIRIKISHO NA YANGA NA FRIENDS RANGERS



TIMU ya Simba itacheza na Burkinafaso na Yanga itacheza na Friends Rangers kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho, mzunguko wa tatu inayotarajiwa kuendelea Januari 12 na Januari 23-27 kwa timu 32 kuchuana kuwania kufuzu kwa hatua ya 16 bora.
Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto alisema mashindano hayo maarufu kama Azam Sports Federation hatua hii itazihusisha timu za ligi kuu.
"Timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu zimeingia moja kwa moja mzunguko wa tatu ambapo zinajumuika na timu 16 zilizofuzu kutoka raundi ya pili yenye timu kutoka ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili", alisema Kizuguto.
Simba itacheza na Burkinafaso,  Januari  23, katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro,  Majimaji itacheza dhidi ya JKT Mlale Uwanja wa Majimaji Songea, Januari 23 Pamba itacheza na Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba na Ndanda FC itaialika Mshikamano kwenye Nag'wanda Sijaona Mtwara.
Young Africans watacheza na Friends Rangers, Januari 24,  Uwanja wa Taifa, Dar es salaam, Njombe Mji watacheza na Tanzania Prisons Uwanja wa Amani Makambako, na Shinyanga Stand United watachuana na Mwadui FC.
Mechi zingine ni Kagera Sugar kucheza na Rhino Rangers, Panone na Madini, Mtibwa Sugar na Abajalo, Lipuli/Kurugenzi na JKT Ruvu, Ashanti United  Azam FC, Africa Sports na Coastal Union, Geita Gold na Mgambo Shooting, Singida United na Mvuvuma na Wenda na Mbeya City.
Timu 15 zilizofuzu hatua ya tatu kutoka raundi ya pili ni Ashanti United, Friends Rangers, Panone, Geita Gold, Pamba, Mvuvuma, Burkinafaso, Rhino Rangers, Madini FC, JKT Mlale, Mshikamano FC, Njombe Mji, Wenda FC, Singida United, Abajalo huku mchezo mmoja kati ya Lipuli dhidi ya Kurugenzi ukichezwa leo hii kusaka timu ya kufuzu raundi ya tatu.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.

No comments:

Post a Comment