Chama cha
soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimeeleza kufurahishwa kwake na ushindi wa tuzo
ya mchezaji bora barani afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za
ndani,aliyoipata mtanzania Mbwana Samatta,baada ya kuwabwaga wenzake wawili kwenye
kinyang’anyiro hicho,akiwemo mchezaji mwenzake wa TP Mazembe,Kipa Robert
Kidiaba pamoja na Mualgeria,Baghdad Boundjah anayeichezea klabu ya Etoile Du
Sahel.
Mwenyekiti wa
DRFA,Almas Kasongo,amesema kamati yake ya utendaji ilianza kuwa na matumaini
makubwa ya Samatta kushinda tuzo hiyo,baada ya kuibuka kuwa mfungaji bora
katika michuano ya klabu bingwa Afrika na kuisaidia timu yake ya TP
Mazembe kutwaa taji hilo kubwa barani Afrika kwa upande wa vilabu.
Kasongo amesema,tuzo
aliyoipata Samatta imechangiwa pia kwa kiasi fulani na usimamizi mzuri wa chama
chake cha mkoa kwa vilabu alivyowahi kucheza kabla ya kujiunga na
Mazembe,ikiwemo African Lyon na Simba SC,ambavyo vyote maskani yake ni jijini
Dar es salaam.
Amesema
Samatta ameandika historia ya aina yake kwa kuipeleka Tanzania katika ramani ya
soka barani afrika,kwa kuwa tuzo hiyo haijawahi kuletwa na mchezaji yeyote yule
kuwahi kutokea hapa nchini.
Kasongo
ameongeza kuwa DRFA,itaendelea kuunga mkono juhudi za wachezaji wote
wanaojituma kusaka mafanikio ndani na nje ya chini,ikiwa ni pamoja na kuunga
mkono juhudi za vyama vingine vya soka vya mikoa katika harakati za kusimamia
na kuharakisha maendelea ya mpira wa miguu kwa faida ya taifa zima.
No comments:
Post a Comment