Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, December 16, 2015

MKUTANO MKUU WA TFF ULIOKUWA UFANYIKE TANGA DESEMBA 19, WAOTA MBAWA 
MKUTANO Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliokuwa ufanyike mwishoni mwa wiki mjini Tanga, sasa hautafanyika tena kutokana na ukosefu wa pesa..
Taarifa kutoka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF zinasema wametumiwa ujumbe mchana huu kutaarifiwa kwamba Mkutano hautakuwepo kwa sababu hakuna fedha kwani bado akaunti zimefungiwa na TRA.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, TRA ilizifunga akaunti zote za TFF kutokana na kukabiliwa na madeni ya kodi za mishahara ya makocha wa timu ya taifa, ‘Taifa Stars’, kuanzia  wakati wa Marcio Maximo, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Mart Nooij.  
Hili linakuwa pigo la pili kwa TFF, baada ya awali kusitisha ziara ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) kwa nchi za Afrika Mashariki.