Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 17, 2015

SERGIO AGUERO APONA, AFANYA MAZOEZI

Embedded image permalinkSTRAIKA  wa Manchester City Sergio Aguero sasa yuko akijifua tayari kurejea kilingeni Jumatatu ijayo huko Emirates Jijini London kuivaaa Arsenal katika Mechi kali kati ya Timu ambazo ziko Nafasi za 2 na za 3 kwenye Ligi Kuu England.
Aguero, Staa wa Kimataifa wa Argentina, amezikosa Mechi 4 zilizopita za Man City baada ya kuumia kifundo cha Mguu lakini amerejea Mazoezini na yupo fiti kucheza Mechi.
Aguero, ambae mapema Msimu huu alikuwa nje kwa Wiki 6 akijiuguza Musuli za Pajani, aliumia kifundo cha Mguu wake Mwezi Novemba wakati City ikiichapa Southampton Bao 3-1.
Kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England, baada ya Mechi 16, Leicester City ndio wako kileleni wakiwa na Pointi 35, wakifuatiwa na Arsenal wenye 33, City 32 na Man United 29.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumamosi Desemba 19

18:00 Chelsea v Sunderland
18:00 Everton v Leicester
18:00 Man United v Norwich
18:00 Southampton v Tottenham
18:00 Stoke v Crystal Palace
18:00 West Brom v Bournemouth
20:30 Newcastle v Aston Villa

Jumapili Desemba 20

16:30 Watford v Liverpool
19:00 Swansea v West Ham

Jumatatu Desemba 21

 23:00 Arsenal v Man City