WATANI wa
Jadi kwenye soka la Tanzania, Simba na Yanga watacheza Septemba 26, mwaka huu
kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Afisa Mkuu wa Bodi ya Ligi,BonifaceWambura, alisema
ligi inatarajiwa kuanza Septemba 12 na kumalizika Mei 7, mwakani.
“Ligi
yetu itaanza kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali hapa nchini na imezingatia
ratiba ya mashindano ya kimataifa, kombe la TFFambalo litaanza Novemba,
uchaguzi mkuu pamoja na ligi daraja la kwanza na imezingatia uwiano wa mechi za
nyumbani na ugenini kwa timu zote”, alisema Wambura.
Kwenye
ratiba iliyotoka jana, Simba atakuwa mwenyeji wa Yanga mchezo wa raundi ya nne
utakaochezwa Uwanja wa Taifa na raundi ya pili watacheza Februari 20, mwakani.
Ligi kuu
msimu huu itashirikisha timu 16 ambapo michezo saba itachezwa siku ya ufunguzi
katika viwanja tofauti ambapo Ndanda wataikaribisha Mgambo Shooting kwenye
uwanja wa Nang’wanda - Mtwara, Simba
watakuwa wageni wa timu ya African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani –
Tanga
Majimajiwataialika
JKT Ruvu Uwanja wa Majimaji - Songea,
Azam FC watawaalika maaskari magereza wa Mbeya Tanzania Prisons kwenye Uwanja
wa Azam Complex, Dsm, huku Stand United wakiivaa Mtibwa Sugar
kwenye Uwanja wa Kambarage – Shinyanga.
Wageni
Toto Africans na Mwadui watakuwa kwenye
kibarua cha kuoneshana na nani bora
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba – Mwanza na Mbeya City wataialika Kagera Sugar
kwenye Uwanja wa Sokoine na Septemba 13, Yanga watakuwa wenyeji wa Coastal
Union Uwanja wa Taifa.
Pia
Wambura alisema wamekagua viwanja vyote ambavyo vitatumika na kukuta karibu
vyote vina mapungufu isipokuwa Azam Complex na Taifa na kuwataarifu wamiliki
kuvifanyia marekebisho kabla ligi kuanza.
“Katika
timu 16 zinazocheza ligi kuu ni timu nne tu zenye viwanja, ambazo ni JKT Ruvu,
Mwadui, Azam FC na Mtibwa na viwanja
vyao havitumiki kwenye michezo inayozihusisha wao na timu za Simba na Yanga
kutokana na kuwa na uwezo mdogo wa kubeba mashabiki na usalama pia”, alisema
Wambura.
Pia
alisema JKT Ruvu watatumia Uwanja wa Karume kama uwanja wao wa nyumbani ila
kwenye mechi na Yanga na Simba watalazimika kutumia Uwanja wa Taifa.
Kutokana
na mwaka huu kuwa na Uchaguzi Mkuu wamewapelekea wamiliki wa viwanja ambavyo
vingi vinamilikiwa na Chama cha Mapinduzi, (CCM) ratiba mapema ili endapo
vitakuwa vikitumika kwa kampeni au shughuli nyingine wawataarifu mapema ili
wafanye mabadiliko kuliko timu kufika na kushindwa kucheza.
Wambura
alimalizia kwa kusema ratiba pia imezingatia haki ya kila mtanzania ya kupiga
kura hivyo wamepisha zoezi hilo kufanyika kiswasawa bila kuwepo na mchezo
weekend hiyo ya Octoba 25.
No comments:
Post a Comment