Andrey Coutinho na Geofrey Mwashiuya |
MASHABIKI wa
Yanga wamemwokoa kiungo Mbrazil Andrey
Coutinho asitemwe Yanga baada ya kumpigia simu Manji na kumtaka mchezaji huyo
aendelee kuwepo kwenye kikosi chao.
Awali baada
ya Yanga kuondolewa kwenye mashindano ya Kagame, Countinho alikuwa aondoke pamoja na beki Mghana, Joseph
Tetteh Zuttah lakini mashabiki walimpigia simu Rais wa Yanga, Yusuph Manji,
wakimtaka mchezaji huyo asiondoke kwenye kikosi kwani kiwango chake kipo juu.
Akizungumza
bila kutaka jina lake kuandikwa gazetini, chanzo hicho kilisema baada ya
mashabiki kusoma na kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa Coutinho anaondoka
waliamua kumpigia simu Manji na yeye kuwasiliana na Katibu Mkuu, Dr. Jonas
Tiboroha akimwambia ahahakishe usajili unafanyika vizuri pia mchezaji huyo
asiondoke.
“Mashabiki
walimpigia simu Manji na yeye akamwagiza Tiboroha awasiliane na benchi la
ufundi kuhakikisha usajili unafanyika vema lakini kiungo Countinho abaki
kuendelea kuichezea Yanga”, kilisema chanzo hicho.
Baada ya
Yanga kutolewa katika robo fainali michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na
Kati, maarufu kama Kombe la Kagame ilikitathmini kikosi chake na kugundua
Zuttah na Coutinho hawana faida.
Coutinho alijiunga na Yanga msimu uliopita
akiletwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Marcio Maximo na hadi sasa ameichezea
timu hiyo mechi 33 na kuifungia mabao sita.
Mbrazil huyo
alikuwa ana wakati mzuri chini ya kocha Maximo, lakini tangu ujio wa Mholanzi,
Hans van der Pluijm amepoteza nafasi katika kikosi cha kwanza.
Tayari Yanga
wamewasajili kiungo Thabani Kamusoko ambaye alikuwa nahodha wa FC Platinum ya
Zimbabwe kuziba nafasi ya Mliberia, Kpah Sherman aliyeuzwa nchini Afrika Kusini
kwenye klabu ya Mpumalanga inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo na beki wa
kimataifa wa Togo, Vincent Bossou ambaye amechukua nafasi ya beki Zuttah.
Wachezaji wa
kigeni Yanga ni Mkongo, Mbuyu Twite, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, Mrundi
Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma.
No comments:
Post a Comment