MENEJA
wa Manchester United Louis van Gaal ameongea na Wanahabari hii Leo
kabla ya Usiku kukutana na Klabu ya Belgium Club Brugge Uwanjani
Old Trafford katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo
ambapo Mshindi wake anatinga hatua ya Makundi na kukiri kuwa ipo presha
kubwa.
Alisema kuwa hana Majeruhi isipokuwa Beki Phil Jones huku Marouane Fellaini yuko huru kucheza kwani Kifungo chake cha Mechi 4 ni cha Mechi za England tu, Van Gaal amesema: “Ipo presha kubwa kwa sababu nia yetu ni kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI na hili ndilo alisema Arsene Wenger Mwaka Jana.”
“Mechi aina hii ni ngumu. Tumepangwa na Brugge na wanajihami vizuri. Pia wanaweza kushambulia, hivyo ni Mechi ngumu na ndio maana presha ni kubwa!”
Mmoja wa Wachezaji hatari wa Club Brugge ni Victor Vasquez, ambae ndie Mchezaji Bora wa Mwaka wa Belgium na pia Kiungo Mshambuliaji, ambae aliwahi kuwa kwenye Timu ya Vijana ya Barcelona wakati Van Gaal ndie Kocha wa Klabu hiyo.
Van Gaal amekiri: “Ni Mchezaji mzuri sana na ni mmoja wa Wachezaji wao muhimu. Si tu ni mwepesi lakini pia ana maarifa.” Van Gaal pia amekiri kutamani kuwepo UEFA CHAMPIONS LIGI kwani hajawahi kuisimamia Klabu kwenye Mashindano hayo tangu aondoke Bayern Munich Mwaka 2011 na anahamu ya kupambana na Klabu nyingine kubwa ikiwa wataitoa Club Brugge.
Amesema: “Ni kweli unakuwa na hamu nayo kwani kama Meneja unataka kuonekana katika jukwaa la juu dhidi ya Klabu za juu.”
Ameongeza: “Kila Timu ya England inaweza kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI au EUROPA LIGI. Nadhani kasi yao ni ya juu kupita kokote Ulaya na Klabu nyingi za Ulaya hazijazoea hilo. Natumai hilo litatunufaisha kuifunga Brugge.”
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumanne Agosti 18
1900 Astana v APOEL Nicosia
BATE Borisov v Partizan Belgrade
Lazio v Bayer Leverkusen
Sporting CP v CSKA Moscow
Manchester United v Club Brugge
Jumatano Agosti 19
Skenderbeu v Dinamo Zagreb
Celtic v Malmo
FC Basel v Maccabi Tel Aviv
Rapid Vienna v Shakhtar Donetsk
Valencia v AS Monaco Marudiano
Jumanne Agosti 25
Dinamo Zagreb v Skenderbeu
Malmo v Celtic
Maccabi Tel Aviv v FC Basel
AS Monaco v Valencia
Shakhtar Donetsk v Rapid Vienna
Jumatano Agosti 26
APOEL Nicosia v Astana
Partizan Belgrade v BATE Borisov
Bayer Leverkusen v Lazio
CSKA Moscowv Sporting CP
Club Brugge v Manchester United

No comments:
Post a Comment