BONDIA
Abdallah Pazi anatarajiwa kupanda ulingoni Idd Pili kwenye ukumbi wa Vijana
Kinondoni kuchuana na Iman Mapambao katika pambano la ubingwa wa Taifa
lililoandaliwa na promota mkongwe Shomari Kimbau chini ya Chama cha Ngumi za
Kulipwa Tanzania (TPBC).
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Kimbau alisema Pazi atapambana na Mapambao katika
uzito wa kilo 76 light heavy raundi 10 ambapo mshindi atapambana na Mkenya
Daniel Wanyonyi katika pambano la Afrika Mashariki litakalofanyika mwezi ujao.
“Maandalizi yanakwenda vizuri, tunategemea
pambano litakuwa la kuvutia kutokana na kuwaleta mabondia vijana wenye uwezo
ambao watakuwa tegemeo baadaye katika mapambano ya kimataifa,”alisema.
Alisema
katika kuboresha na kuhamasisha michezo mshindi wa pambano hilo la ubingwa
atavalishwa mkanda wa taifa na Diwani wa Kata ya Mwananyamala Songoro Mnyonge.
Aidha,
aliwataja mabondia wasindikizaji kuwa ni Rahim Maokola atachuana dhidi ya George
Demoso uzito wa kilo 60 L/middle,
Shabani Kaoneka dhidi ya Sweet Kalulu
uzito wa kilo 72 middle weight raundi nane na Chid Mbishi dhidi ya Mbwana Mdani uzito wa kilo 52 Flyweight raundi sita.
Wengine ni
Aman Mssy dhidi ya Peter Nunda uzito wa kilo 86 heavyweight raundi nne na Hans
Mawe dhidi ya Bakari Chuma wenye uzito sawa na huo.
Kimbau
alisema amerudi kwenye ngumi baada ya kuona kuwa TPBC imesajiliwa chini ya
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kuwasaidia mabondia chipukizi kutimiza
ndoto zao.
“Nawashukuru
sana BMT kwa kuisajili TPBC kwani kufanya hivyo ni kutambua na kuunga mkono
kazi ambazo tumekuwa tukizifanya katika kuendelea mchezo wa ngumi nchini,
tunakuja kwa kasi kuandaa mapambano mbalimbali ili kuibua wengine
wasiofahamika,”alisema.
Alisema yeye
ndiye aliwaibua mabondia wakubwa kama Kalama Nyilawila na Mada Maugo hivyo
kitendo cha kurudisha kasi kwa mabondia hao chipukizi kutawaimarisha viwango
vyao.
Alisema
baada ya pambano hilo, anatarajia kuandaa mengine nane na kushirikisha mabondia tofauti
kwa lengo la kupata mabondia 10 bora.
No comments:
Post a Comment