Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 20, 2015

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: DROO YA ROBO FAINALI KUFANYIKA LEO

Droo ya kupanga Mechi za Robo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI itafanyika leo Machi 20 huko Nyon, Uswisi kuanzia Saa 8 Mchana kwa muda wetu.
Klabu 8 kutoka Nchi 5 za Ulaya zipo kwenye Droo hiyo ambayo tofauti na Raundi zilizopita, safari hii Droo hii ni huru na hivyo Klabu za Nchi moja hazibaguliwi na zinaweza kukutanishwa.
Hivyo, safari hii upo uwezekano kuwepo kwa El Clasico ya Ulaya kwa Mahasimu Mabingwa Watetezi Real Madrid kupambanishwa na FC Barcelona.
Mechi za Robo Fainali zitachezwa hapo Aprili 14 na 15 na Marudiano ni Aprili 21 na 22.
Droo ya Nusu Fainali itafanyika Aprili 24 na Mechi zake kuchezwa Mei 5 na 6 na Marudiano ni Mei 12 na 13.
Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI itachezwa hapoJumamosi Juni 6 huko Olympiastadion, Jinini Berlin, Ujerumani.


WALIOTINGA HATUA YA ROBO FAINALI:
Club Atlético de Madrid (ESP)
FC Barcelona (ESP)
FC Bayern München (GER)
Juventus (ITA)
AS Monaco FC (FRA)
Paris Saint-Germain (FRA)
FC Porto (POR)
Real Madrid CF (ESP, holders)


 
NJIA NYEUPE BERLIN
Quarter-finals: Draw 20 March, matches 14-15 & 21-22 April
Semi-finals: Draw 24 April, matches 5-6 May & 12-13 May
Final: Saturday 6 June