Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, March 18, 2015

SIMBA YASHINDWA KUNGURUMA MKWAKWANI TANGA





SIMBA SC imepunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, baada ya kufungwa mabao 2-0 na Mgambo Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga leo.

Matokeo hayo yanazidi kuondoa matumaini ya Simba SC inayofundishwa na Mserbia, Goran Kopunovic siyo tu kutwaa ubingwa, bali hata kushika nafasi ya pili. 

Mgambo ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa mchezaji wa zamani wa Coastal Union ya Tanga pia, Ally Nassor ‘Ufudu’ aliyemalizia krosi ya Fully Maganga.

Mapema dakika ya 21, Emmanuel Okwi aliikosesha Simba SC bao la wazi, baada ya kushindwa kuunganisha krosi nzuri ya Ibrahim Ajib na dakika ya 35.

Kipindi cha pili ndipo jahazi la Simba lilipozama kabisa, baada ya kuongezwa bao la pili lililofungwa na Malimi Busungu kwa penalti dakika ya 66, baada ya kipa Ivo Mapunda kumchezea rafu Fully Mganga aliyekuwa anakwenda kufunga.

Ivo alitolewa kwa kadi nyekundu na refa Amon Paul kutoka Mara, na Simba SC ikamuingiza kipa Peter Manyika kwenda kuchukua nafasi ya Said Ndemla.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohammed ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Abdi Banda, Said Ndemla/Peter Manyika dk66, Ibrahim Hajibu/Elias Maguri dk46, Emmanuel Okwi/Simon Sserunkuma dk79 na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Mgambo Shooting; Godson Mmasa/Said Lubawa dk60, Bashiru Chanache, Salim Mlima, Salim Kipanga, Ramadhani Malima, Novaty Lufunga, Mohammed Samatta, Ally Nassor, Fully Maganga, Malima Busungu na Salim Aziz Gilla.

No comments:

Post a Comment