Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 8, 2015

JONNY EVANS AFUNGIWA MECHI 6, CISSE MECHI 7 KWA KUTEMEANA MATE UWANJANI


BEKI wa Manchester United Jonny Evans na Fowadi wa Newcastle Papiss Cisse wameshushiwa Vifungo vikali kwa Kosa la kumeana mate wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England Jumatano iliyopita Uwanjani St James Park ambayo Man United walishinda 1-0.
Cisse, ambae alikiri Kosa lake, amefungiwa Mechi 6 pamoja na moja ya ziada kwa vile Msimu huu tayari alishawahi kuwa Kifungoni wakati Evans, aliekanusha Shitaka lake, amefungiwa Mechi 6. Tukio hilo, ambalo halikuonwa na Refa, lilitokea Dakika ya 38 ya Gemu hiyo ambapo Evans alimvaa Cisse alieanguka chini na Evans kuonekana akitema mate upande wa Cisse ambae baada ya kuinuka alimtemea mate Evans shingoni.
Kabla ya FA kutangaza kufungua Mashitaka dhidi yao, Papiss Cisse alimwomba radhi Jonny Evans pamoja na Wadau wa Soka lakini, Evans alikanusha kukusudia kumtemea mate Cisse na kudai si hulka yake kufanya kitendo cha aina hiyo.
FA, Chama cha Soka cha England, kimedai Kosa hilo ni kinyume na Sheria yao E1[a].

No comments:

Post a Comment