Timu ya Simba Sc imeibuka kidedea
kwa kutwaa kombe la mapinduzi kwa mikwaju 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar
katika mchezo ulipigwa kwenye dimba la Amaani Visiwani Zanzibar.
Penati za simba zilifugwa na Awadh Juma, Hassan Kessy, Hassan Isihaka na Dan Ssenrukuma wakati ya Shaaban Kisiga iliokolewa na Kipa Said Mohamed.
Penati za Mtibwa Sugar zilifungwa na Ally Lundenga, Shaaban Nditi na Ramadhan Kichuya huku Ibrahim Rajab ikigonga mwamba huku penati ya Vincent Barnabas ikiokolewa na kipa Ivo Mapunda.
Nahodha wa Simba, Hassan Isihaka,alikabidhiwa Kombe la Mapinduzi pamoja na Shilingi Milioni 10 kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohammed Shein.
Kipa Said Mohammed wa Mtibwa Sugar amekuwa kipa bora wa michuano,beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde ameibuka kuwa mchezaji bora wa michuano.Mfungaji bora amekuwa Simon Msuva wa Yanga ambaye alifunga mabao manne.
Wekundu
wa msimbazi ‘Simba Sc’ wamefanikiwa kunyakua kombe la Mapinduzi baada
ya kuilaza Mtibwa Sukari ya Morogoro kwa mikwaju ya penalti katika
fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Amani visiwani Zanzibar usiku wa
kuamkia leo(Jan.13).
Mpaka dakika 90 zinamalizika sio Simba wala Mtibwa ambaye alifanikiwa kutikisa nyavu za mwenzake. Kipa wa Simba, Ivo Mapunda ameweza kuibuka shujaa wa mchezo huo baada ya kufuta mikwaju miwili ambayo ilipigwa na Rajab Jeba pamoja na Vicent Barnabas wote wa Mtibwa baada ya kuchukua nafasi ya golikipa Peter Manyika mnamo dakika ya 90.
Wakati kwa upande wa Simba wakipoteza mkwaju mmoja uliopigwa na Shabani Kisiga na kufanya matokeo kumalizika kwa wekundu hao wa msimbazi kuibuka bingwa kwa jumla ya mikwaju minne ya penalti dhidi ya mitatu.
Kwa matokea hayo yanaifanya timu ya Simba kuendelea kushikilia rekodi yake ya kuifunga Mtibwa mara mbili katika michuano hiyo ya Mapinduzi.
Simba Sc walikabidhiwa kombe lao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Ali Mohammed Shein na zawadi ya shilingi milioni 10 kwa kutwaa ubingwa, wakati Mtibwa ikiambulia shilingi milioni 5 za kibongo kama zawadi ya mshindi wa pili.
Wachezaji wa Timu Simba wakishangilia Ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi baada ya kushinda Mchezo wa Fainali na Timu ya Mtibwa kwa kuifunga 4-3
MIKWAJU YA PENATI
SIMBA: 1, X,1,1,1
MTIBWA SUGAR: 1, 1,X,1,X
Kipa Mapunda aonesha kiwango langoni..
Mshambuliaji wa timu ya Simba Ramadhani Shindano Messi, akimpita beki wa
timu ya Mtibwa Sugar wakati wa mchezo wao wa Fainal ya Kombe la
Mapinduzi uliofanyika usiku huu uwanja wa Amaan, Timu ya Simba imeshinda
kwa penenti 4--3
Wapenzi wa mchezo wa mpira Zanzibar wakifuatilia mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi liofanyika usiku huu uwanja wa amaan Zanzibar timu ya Simba imeshinda mchezo huo na kuwa Bingwa kwa mwaka 2015 bingwa Mapinduzi Cup.
Mshambuliaji wa timu ya Simba Emanuel Okwi, akimpita beki wa timu ya Mtibwa wakati wa mchezo wao wa fainali ya Kombre la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa amaan.
Mshambuliaji wa timu ya Mtibwa akimpita beki wa timu ya Simba katika mchezo wa fainali ya Kombev la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar usiku huu.
Mashabiki wa Simba
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa na majongo wakati wa mchezo wa timu ya Mtibwa kuwa sare wakati wa kipindi cha pili kumaliziki hawaamie kama mchezo umemalizika kwa sare ya bila kufungana na kupigiana penenti Simba imeshinda 4 na kukosa moja wakati Mtibwa wameshinda 3 na kukosa mbili
Kikosi cha Mtibwa Sugar ya Morogoro
Kipindi cha kwanza kimemalizika cha dakika 45, mpira ni mapumziko...Hakuna aliyeliona lango lango la mwenzake katika kipindi cha kwanza.
Kikosi cha Timu ya Simba Sc
Mpaka dakika 90 zinamalizika sio Simba wala Mtibwa ambaye alifanikiwa kutikisa nyavu za mwenzake. Kipa wa Simba, Ivo Mapunda ameweza kuibuka shujaa wa mchezo huo baada ya kufuta mikwaju miwili ambayo ilipigwa na Rajab Jeba pamoja na Vicent Barnabas wote wa Mtibwa baada ya kuchukua nafasi ya golikipa Peter Manyika mnamo dakika ya 90.
Wakati kwa upande wa Simba wakipoteza mkwaju mmoja uliopigwa na Shabani Kisiga na kufanya matokeo kumalizika kwa wekundu hao wa msimbazi kuibuka bingwa kwa jumla ya mikwaju minne ya penalti dhidi ya mitatu.
Kwa matokea hayo yanaifanya timu ya Simba kuendelea kushikilia rekodi yake ya kuifunga Mtibwa mara mbili katika michuano hiyo ya Mapinduzi.
Simba Sc walikabidhiwa kombe lao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Ali Mohammed Shein na zawadi ya shilingi milioni 10 kwa kutwaa ubingwa, wakati Mtibwa ikiambulia shilingi milioni 5 za kibongo kama zawadi ya mshindi wa pili.
Wachezaji wa Timu Simba wakishangilia Ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi baada ya kushinda Mchezo wa Fainali na Timu ya Mtibwa kwa kuifunga 4-3
MIKWAJU YA PENATI
SIMBA: 1, X,1,1,1
MTIBWA SUGAR: 1, 1,X,1,X
Kipa Mapunda aonesha kiwango langoni..
Wapenzi wa mchezo wa mpira Zanzibar wakifuatilia mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi liofanyika usiku huu uwanja wa amaan Zanzibar timu ya Simba imeshinda mchezo huo na kuwa Bingwa kwa mwaka 2015 bingwa Mapinduzi Cup.
Mshambuliaji wa timu ya Simba Emanuel Okwi, akimpita beki wa timu ya Mtibwa wakati wa mchezo wao wa fainali ya Kombre la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa amaan.
Mshambuliaji wa timu ya Mtibwa akimpita beki wa timu ya Simba katika mchezo wa fainali ya Kombev la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar usiku huu.
Mashabiki wa Simba
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa na majongo wakati wa mchezo wa timu ya Mtibwa kuwa sare wakati wa kipindi cha pili kumaliziki hawaamie kama mchezo umemalizika kwa sare ya bila kufungana na kupigiana penenti Simba imeshinda 4 na kukosa moja wakati Mtibwa wameshinda 3 na kukosa mbili
Kikosi cha Mtibwa Sugar ya Morogoro
Kipindi cha kwanza kimemalizika cha dakika 45, mpira ni mapumziko...Hakuna aliyeliona lango lango la mwenzake katika kipindi cha kwanza.
Kikosi cha Timu ya Simba Sc
No comments:
Post a Comment