

Bao la pili la Man City lilifungwa dakika za majeruhi dakika ya 86 na Pablo Zabaleta baada ya kupewa pasi na Samir Nasri.



Kwenye Kundi E tayari Bayern Munich wameshafuzu na kuacha kinyang’anyiro cha Timu ipi itaungana nayo kwa Timu 3 zilizobakia ambazo ni AS Roma, Man City na CSKA Moscow.
Timu zote hizo 3 zina Pointi 5 kila mmoja lakini nani ataungana na Bayern ni kitendawili kikubwa hasa ukichukulia Kanuni za UEFA hupima matokeo ya Uso kwa Uso kwa Timu zilizofungana Pointi.
Kati ya Timu hizo 3 hatima ya AS Roma iko mikononi mwao wenyewe kwani wakiifunga City wao watafuzu.

AS Roma wakitoka Droo na City inaweza ikawasaidia na pia inaweza ikawaua ikitegemea CSKA wamefanya nini kwenye Mechi yao Mjini Munich na Bayern Munich.
CSKA wao wanaweza kufuzu ikiwa wataifunga Bayern huku AS Roma ikishindwa kuifunga City.
City watafuzu wakiifunga Roma na CSKA kutoshinda.
Lakini Mahesabu yatakuwa magumu pale Mechi ya City na Roma kuwa Sare.
RATIBA
Jumatano Desemba 10
KUNDI E
Bayern Munich vs CSKA Moscow
AS Roma vs Man City
KUNDI F
Ajax v Apoel Nicosia
Barcelona v Paris Saint Germaine
KUNDI G
Chelsea v Sporting Lisbon
NK Maribor v Schalke
KUNDI H
Athletic Bilbao v BATE Borisov
FC Porto v Shakhtar Donetsk
No comments:
Post a Comment