Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, Usiku huu wameibwaga Timu ya
Daraja la chini yake Championship, Derby County, Bao 3-1 kwenye Kombe la
Ligi, Capital One Cup kama linavyojulikana sasa, na kutinga Nusu
Fainali.
Filipe Luis aliifungia bao la pili
dakika ya 56 na kufanya 2-0 dhidi ya Derby kwa frii kiki iliyozama moja
kwa moja langoni mwao.Bao za Chelsea kwenye Mechi hii ambayo Derby walibaki Mtu 10 baada ya Jake Buxton kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 78 zilifungwa na Eden Hazard, Dakika ya 23, Filipe Kuis, 56, na Andre Schurrle, 82.
Bao la Derby lilifungwa na Craig Bryson Dakika ya 71. Kipa Petr Cech, Kurt Zouma na Mchezaji wa Derby Richard Keogh kwenye patashika
Difenda wa Chelsea Zouma aliumia baada ya kukutana na kiwiko cha mkono wa Kipa wake Cech.
Dokta wa Timu ya Chelsea wakitoa huduma ya kwanza kwa mchezaji wa Chelsea Kurt Zouma aliyeumia akigombea mpira baada ya kuruka na kupigwa kiwiko na Kipa Petr Cech, Richard Keogh mchezaji wa Derby nae alikuwemo kwenye patashika hiyo iliyosababisha Zouma kuumia.
Cesar Azpilicueta na Cesc Fabregas wakisaidia kumtoa haraka mchezaji wao kwenda kupata matibabu ya haraka nje ya Uwanja.
Kwenye Mechi nyingine ya Robo Fainali zilizokuwa zinapigwa kwa wakati mmoja Sheffield United, inayocheza Daraja la Ligi 1 likiwa ni Daraja la chini ya Championship, iliifunga Timu ya Ligi Kuu England, Southampton Bao 1-0.
Bao la ushindi la Sheffield lilifungwa na McNulty Dakika ya 63 na Southampton kubaki Mtu 10 baada ya Gardos kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 90.
Leo Usiku zitachezwa Robo Fainali nyingine mbili ambapo Liverpool watakuwa Wageni wa Bournemouth ambao ndio Vinara wa Daraja la Championship na Mechi nyingine ni ile pekee ya Timu za Ligi Kuu England itakayochezwa White Hart Lane Jijini London kati ya Tottenham Hotspur na Newcastle United.Red!
1-0Eden Hazard dakika ya 23 kipindi cha kwanza aliifungia bao Chelsea na hapa akipongezwa kwa bao hilo dhidi ya Derby County.
Derby County vs Chelsea
No comments:
Post a Comment