WENGER ATIMKIA ITALIA KWENDA KUCHEZESHA MECHI YA HISANI WAKATI WENZAKE WAKIHAHA NA USAJILI WA DAKIKA ZA MWISHO
WAKATI hekaheka za
usajili zikiendelea kushika kasi katika kipindi hiki cha mwisho, meneja
wa Arsenal Arsene Wenger yeye atatumia muda huu wa saa chache uliobakia
kabla ya dirisha la usajili kufungwa jijini Rome akiwa kama mwamuzi wa
mechi hisani.
Mfaransa huyop alisafiri kwenda Italia kwa ajili ya mechi
iliyoandaliwa maalumu kuhamasisha amani itakayofanyika katika Uwanja wa
Olimpiki ambapo baadhi ya nyota kama Andrea Pirlo, Samuel Eto’o,
Ronaldinho, Gianluigi Buffon, Diego Maradona, Paulo Maldini na Andriy
Schevchenko watakuwwepo katika mchezo huo.
Chanzo kimoja cha habari
kutoka ndani ya klabu hiyo kimesisitiza kuwa kutokuwepo kwa Wenger
hakutaathiri kwa vyovyote uwezo wao wa kusajili katika muda wa
mwisho.
Hata hivyo inafahamika kuwa katika muda huu wa mwisho Arsenal
wametupa ndoano yao kwa Matija Nastasic, Weinston Reid na Ron Vlaar ili
mmoja wao aje azibe nafasi ya Thomas Vermaelen.
Kwa upande wa
ushambuliaji Wenger anaonekana kama ameridhika na aliokuwa nao pamoja na
kuumia kwa Olivier Giroud baada ya kuwakosa Loic Remy aliyekwenda
Chelsea na Radamel Falcao aliyekwenda Manchester United kwa mkopo wa
mwaka mmoja.
Kuna uwezekano wa Arsenal kusajili mchezaji mmoja au wawili
kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili lakini haidhaniwi kama
atasajili mshambuliaji tena pamoja na upungufu aliokuwa nao katika safu
hiyo.
No comments:
Post a Comment