Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, September 23, 2014

MANCHESTER UNITED KIPIGO CHA 5-3, WACHAMBUZI WADAI REFA CLATTENBURG ALICHANGIA

BAADA ya Jana kuongoza Bao 3-1 huko King Power Stadium katika Mechi ya Ligi Kuu England, Manchester United walijikuta wakibondwa 5-3 na Leicester City huku Refa Mark Clattenburg akilaumiwa sana kwa Penati ‘tata’ iliyozaa Bao la Pili la Leicester City.
Hazikudumu hata Dakika 2 baada ya Penati hiyo kutolewa, Leicester City wakasawazisha na kisha kuongeza Bao 2 nyingine, moja likiwa la Penati nyingine iliyosababisha pia Beki wa Man United Chipukizi Tyler Blackett kupewa Kadi Nyekundu.Wachambuzi huko England wamedai Penati iliyozaa Bao la Pili kwa Leicester ndiyo ilibadili Gemu na haikustahili kabisa.
Msimamo huo umeungwa mkono na aliekuwa Refa mkubwa huko England, Graham Poll, ambae alidai Refa Mark Clattenburg alikosea kabisa kuwapa Penati hiyo Leicester City.

Poll alidai Refa huyo alipaswa kutoa Rafu baada ya Fowadi wa Leicester, Jamie Vardy, kumsukuma Rafael, na mbali ya hiyo, kitendo cha baadae ya tukio hilo pale Rafael alipoinuka na kumkabili tena Vardy ambae safari hii akajiangusha yeye, hakikustahili kabisa Penati.
Mbali ya utata huo, Wachambuzi pia wamenyooshea kidole Difensi mbovu ya Man United kwa kuruhusu Bao 3, ukiondoa hizo Penati mbili, za laini kabisa katika Mechi ambayo ukweli waliitawala na kuwa na kila sababu ya kushinda hasa baada ya kuwa Goli 3-1 mbele.
Pengine, Man United watajutia sana kwa nini hawakusaini Madifendi maarufu waliojengeka pamoja na Kiungo Mkabaji mkali katika Kipindi cha Usajili wa Mwezi Julai.Mwamuzi mwenyewe yupo nyuma..mpira upo mbele..kwa maana kama upo nje ya Uwanja! wakakausha!Di Maria akiwa chini anajiuguza..baada ya kusukumwa nje na Refa kupeta..Balaa lilianzia hapa...2-34-35-3Tyler Blackett alioneshwa Kadi nyekundu kwa rafu hii

No comments:

Post a Comment