Cristiano
Ronaldo alifanikiwa kumshinda Lionel Messi katika tuzo ya mchezaji bora
wa dunia ya Ballon d'Or mapema mwaka huu, lakini mshambuliaji huyo wa
Barcelona amelipiza kisasi kwa mshindani wake mkubwa wa kizazi cha sasa
katika soka kupitia shindano lingine la FIFA la wachezaji bora 15 'video game'.
Akiwa
amepata alama 93 kati ya 100, Messi ameongoza katika orodha ya
mlinganisho wa ubora wa wachezaji kupitia mchezo wa video (yaani video
game) wa shirikishp la soka duniani FIFA maarufu kama 'video game FIFA
15', ambao matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa septemba 26 nchini
Uingereza.
Ili
kuweza kumaliza ubishi kwa mashabiki watengenezaji wa mchezo huo
kampuni ya EA Sports imeweka orodha ya wachezaji 50 katika mchezo mpya
kusaka wachezaji bora ambao wanaangaliwa kwa njia ya teknolojia ya video
ambao utahusishwa watu wengi kuwezesha kutoa maoni yao.
Barcelona wana uhakika kupitia mchezo huu watu wengi watampa Messi kushinda
Nyota wa Argentina(kulia) alianza msimu kwa kiwango cha kuvutia
Anayefuatia kwa ubora: Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amepewa 92 katika FIFA 15
Hatari: EA Sports wamekadiria uwezo wa kupiga mpira wa Ronaldo na kupata kura 93 kati ya 100
Kubwa
ambalo linazingatiwa katika kukadiria ubora wa mchezaji ni kwamba na
hatimaye kutinga katika orodha ya wachezaji 15 bora kupitia shindano
hili, inazingatiwa uwezo wako binafsi, uwezo wa kupiga mipira, kukokota
mpita, idadi na upigaji wako wa pasi, kuzuia wapinzani na hata kufunga
magoli.
ORODHA KAMILI FIFA 15 TOP 10 PLAYERS
1. Lionel Messi 93
2. Cristiano Ronaldo 92
3. Arjen Robben 90
4. Zlatan Ibrahimovic 90
5. Manuel Neuer 90
6. Andres Iniesta 89
7. Luis Suarez 89
8. Bastian Schweinsteiger 88
9. Franck Ribery 88
10. Eden Hazard 88
Katika
orodha ya wachezaji 50 kuna idadi kubwa ya wachezaji kutoka katika
klabu ya Bayern Munich ikiwa na jumla ya wachezaji 11, huku Real Madrid
ikiwa na wachezaji 8.
Barcelona imeingiza wachezaji 6 akiwemo mchezaji bora wa mchezo huu mpya Lionel Messi.
Kwa
upande wa klabu za Premier League Manchester United imeongoza ikiwa pia
imeingiza wachezaji wake wapya Radamel Falcao na Angel Di
Maria.
Kikosi cha Louis van Gaal jumla kimeingiza wachezaji 5 katika wachezaji 50 wakiwemo Juan Mata, Wayne Rooney na Robin van Persie.
Chelsea pia imeingiza wachezaji 5 akiwemo alisajiliwa kiangazi Diego Costa na Cesc
Fabregas wakati ambapo Manchester City imeingiza wachezaji wanne tu kufuatia kuondoka kwa Jesus Navas.
Arsenal na Tottenham zote zimeingiza mchezaji mmoja kila moja Mesut Ozil na Hugo Lloris wakati ambapo Luis
Suarez akiingia katika orodha hata baada ya kuihama Liverpool.
No comments:
Post a Comment