Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, September 24, 2014

ANFIELD YAPASISHWA KUPANULIWA, VITI 13,000 KUONGEZWA, KUTOKA WATU 45,500 - 59,000.


Anfield could look like this should its potential 13,000 seats be added to bring its capacity to about 58,800KLABU ya Liverpool imepata Kibali cha kuiruhusu kupanua Uwanja wao wa Anfield kutoka kuchukua uwezo wa Watu 45,500 hadi Watu 59,000 na ujenzi huo utagharimu Pauni Milioni 100.Liverpool's new Main Stand will be made up of three tiers and will include premium seating for Reds fans
Halmashauri ya Jiji la Liverpool limeipa Klabu ya Liverpool Kibali cha ujenzi ambao utawawezesha kupanua Jukwaa Kuu la Uwanja huo na kuchukua Watu 8,300 zaidi na Jukwaa la Barabara ya Anfield kuongezwa na kubeba Watu 4,800 zaidi.
Upanuzi wa Anfield unatarajiwa kuanza Mwakani na kukamilika kabla ya Msimu wa 2016/17.
Anfield is soon to be altered after Liverpool Football Club won permission from the city council on Tuesday
Mapendekezo ya Liverpool ya upanuzi wa Uwanja huo yanahusu kulifanya Jukwaa Kuu liwe na ngazi mbili za Watazamaji wanaokaa Vitini na pia kuongeza sehemu za Mikutano na Hoteli, sehemu za Duka la Klabu na kupanua sehemu ya kuegesha Magari.
Liverpool Football Club is soon to add more seats to its famous and iconic home Anfield - to look like this
Katika Maombi yao ya upanuzi wa Anfield, Klabu ya Liverpool ilisema upanuzi huo umelenga Klabu yao kuweza kuwa Wenyeji wa Mashindano makubwa ya Kimataifa na Fainali za Ulaya.

Klabu hiyo ilieleza hivi sasa Anfield iko chini ya Viwango vya UEFA na Ligi Kuu England ambavyo vimeizuia Klabu hiyo kuwa Wenyeji wa Mashindano makubwa.
This current aerial view of Anfield is soon to change after Liverpool Football Club won permission
Mojawapo ya Viwango vya UEFA kwa Uwanja kupewa Mechi za Kimataifa ni uwezo wa Uwanja kuchukua Watu si chini ya 50,000 na kuwa na sehemu za kuridhisha za Watu muhimu pamoja na Vyumba vya Kubadili Jezi kwa Wachezaji na Marefa veynye kukidhi mahitaji ya msingi kwa viwango maalum.

Hata hivyo uamuzi huu wa Halmashauri ya Jiji la Liverpool kuipa Klabu ya Liverpool Kibali cha ujenzi umezua upinzani toka baadhi ya Wananchi wa Jiji la Liverpool wanaodai upanuzi huo utalichafua Jiji na kuzidisha msongamano.


VIWANJA VINGINE VINAVYOONGOZA KWA KUINGIZA WATU WENGI LIGI KUU ENGLAND NI KAMA:
1. 75,731 - Old Trafford, Manchester United
2. 60,362 - Emirates Stadium, Arsenal
3. 52,405 - St James' Park, Newcastle United
4. 48,707 - Stadium of Light, Sunderland
5. 46,708 - Etihad Stadium, Manchester City
6. 45,522 - Anfield, Liverpool

No comments:

Post a Comment