Katibu wa Mbeya City Emmanuel Kimbe |
Uongozi wa klabu ya Mbeya City umesema huenda ukasitisha zoezi la usajili katika kipindi hiki kutokana na sera waliyojipangia ya kutaka kuwapandisha baadhi ya wachezaji wa timu yao ya vijana.
Akiongea na Rockersports katibu mkuu wa Mbeya City Emmanuel Kimbe amesema mpaka sasa wameshakamilisha usajili wa wachezaji wawili, ambao walipendekezwa na kocha wao Juma Mwambusi na kinachoendelea sasa ni wanaagalia namna ya kuwapandisha wachezajia wa kikosi cha pili cha klabu hiyo ambao wanaweza kutoa mchango mkubwa katika kikosi cha wakubwa.
Aidha Kimbe amaezungumzia suala la mabadiliko ya watendaji wa klabu hiyo mabadiliko ambayo huenda yafanyika katika kipindi hiki, kufuatia baadhi ya watumishi wao kumaliza mikataba yao.
No comments:
Post a Comment