Na Faustine Ruta, Bukoba
Ligi Kuu Vodacom imeendelea leo na Hapa Mjini Bukoba tukishuhudia Timu ya Maafande kutoka Jijini Mbeya imenyukwa bao 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar. Kipindi cha kwanza Tanzania Prisons ndio walipata bao kupitia kwa mchezaji wao Peter Michael dakika ya 37 baada ya kuwachambua mabeki wa Kagera Sugar na kuachia shuti kali na kumfunga kipa wa Kagera Sugar.
Mpaka dakika za mapumziko Tanzania Prisons ndio wameenda kupumzika wakiwa mbele ya Bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar.
Kipindi cha pili dakika ya 55 Kagera Sugar walipata penati na mkwaju huo ulipigwa na Salum Kanoni na kupata bao la kusawazisha. Katika dakika za lala salama dakika ya 88 Kagera Sugar walipata bao la ushindi lililofungwa na Benjamini Asukire kwa shuti kali ndani ya eneo hatari la penati nakufanikisha Timu yao kuibuka na ushindi wa bao hizo mbili.
Wachezaji wa Kagera Sugar wakipongezana kipindi cha pili baada ya mwenzao Benjamini kupata bao la pili
Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, David Mwamwaja hoi baada ya kupigwa bao la pili!!
Mchezaji wa Kagera Sugar Benjamini Asukire akishangilia bao lake!
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja ambaye ni raia waUganda akiwaelekeza wachezaji wake baada ya timu hiyo kupata bao la pili.
Dakika za nyongeza zikamalizika, Na hapa ni Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja akishangilia Ushindi kwa timu yake Kagera Sugar
Yes Yes yes yes yeeees!!!!!! Ni Furaha za Kocha Jackson Mayanja
Aliyeipatia bao la ushindi kagera nae kwenye Kamera!! ni Benjamini Asukire(kulia)
No comments:
Post a Comment