Shirikisho la Mpira wa Miguu
barani Afrika CAF leo tarehe 31 Januari 2014 limeupa kibali cha kuchezea
mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na CAF uwanja wa Azam Complex Chamazi na
kuufanya uwanja wa kwanza unaomilikiwa na klabu Afrika Mashariki kuruhusiwa kuandaa (ku-host) mashindano
makubwa ya vilabu
Kwa mujibu wa barua pepe
iliyotumwa leo na CAF kupitia kwa naibu mkurugenzi wa mashindano Bwana
Khaled Nassar, Uwanja wa Azam Compex Chamazi umepita vigezo vyote
vinavyohitajika na CAF “ku-host” mashindano yakimataifa hivyo kuanzia tarehe ya
leo, uwanja huu unaruhusiwa “ku-host” mech za CAF
Bwana Khaled ameandika katika
taarifa yake ya barua pepe kwenda TFF na Azam FC kuwa CAF ilimtuma mkaguziwake
toka nchini Zimbabwe Bwana Wilfried Mukuna kuja kukagua uwanja huu. Bwana
Mukuna aliwasilisha ripotiCAF iliyopelekea shirikisho hilo kutoa kibali kwa
Azam FC na TFF kuruhusiwa kuutumia uwanja huu kwa mechizinazoandaliwa na CAF
Uongozi wa Azam FC unatoa
shukrani kwa mkaguzi wa CAF Bwana Mukuna, Uongozi wa TFF chini ya Rais
JamalMalinzi, na uongozi wa CAF Cairo Misri hasa Bwana Khaled Nasser kwa
kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa uwazina uweledi wa hali ya juu uliopelekea
uwanja wetu kupata kibali cha kutumika kwenye michezo ya kimataifa.
Azam FC ingependa kuwataarifu
wapenzi wake kuwa kuanzia msimu huu mechi zake za CAF zitachezwa AzamComplex Chamazi
No comments:
Post a Comment