Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya uteuzi wa wajumbe kuunda kamati mbili za awali za haki, na kamati mbili za rufani za vyombo hivyo.
Rais
wa zamani wa Yanga, Tarimba Abbas ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria ataongoza
Kamati ya Nidhamu. Wajumbe wanaounda kamati hiyo ni Wakili Jerome Msemwa (Makamu
Mwenyekiti), Kassim Dau, Nassoro Duduma na Kitwana Manara.
Kamati
ya Rufani ya Nidhamu inaendelea kuongozwa na Profesa Mgongo Fimbo wakati makamu
wake ni Wakili Hamidu Mbwezeleni. Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Titus
Bandawe, Twaha Mtengera na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface
Mpaze.
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, William Erio ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria anaongoza Kamati
ya Maadili. Wajumbe ni Wakili Ezekiel Maganja, Wakili Victoria Mandari, Kanali
mstaafu Enos Mfuru na Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Said Mtanda.
Kamati
ya Rufani ya Maadili inaundwa na Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti),
Wakili Alesia Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na
Chabanga Hassan Dyamwale.
No comments:
Post a Comment