Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Yanga na Mbeya City lililofanyika
jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh.
175,285,000.
Watazamaji
30,411 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio sh. 5,000, sh.
15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Yanga ndiyo iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mgawanyo
wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 26,738,389.83, gharama
za kuchapa tiketi sh. 2,919,200 wakati kila klabu ilipata sh. 42,960,086.50.
Uwanja
sh. 21,844,111.53, gharama za mechi sh. 13,106,466.92, Bodi ya Ligi sh. 13,106,466.92,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,553,233.46 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,096,959.36.
Nayo
mechi ya Simba na Oljoro JKT iliyochezwa Februari 1 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 47,705,000 ambapo kila timu imepata sh.
11,254,122 kutokana na watazamaji 8,267.
Mgawanyo
mwingine katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 4-0 ni Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 7,277,033.90 na gharama za kuchapa tiketi sh.
2,278,400.
Uwanja
sh. 5,722,434.92, gharama za mechi sh. 3,433,460.95, Bodi ya Ligi sh. 3,433,460.95,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,716,730.47 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,335,234.81.
No comments:
Post a Comment