Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri yake kwenye mechi
yake ya kwanza ya raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly
kutoka Misri.
Mechi
hiyo inachezwa kesho (Machi 1 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia
10 kamili jioni. Timu hizo zitarudiana Machi 9 mwaka huu jijini Cairo, Misri.
Maandalizi
ya mechi hiyo yamekamilika ambapo kamishna Abbas Sendyowa kutoka Uganda na
waamuzi wanne kutoka Burundi tayari wapo nchini kwa ajili ya mechi hiyo
inayotarajiwa kuvuta maelfu ya washabiki.
Milango
yote katika uwanja huo itakuwa wazi, ukiwemo ule wa upande wa Uwanja wa Ndani
(Indoor Stadium) wakati Barabara ya Taifa (Taifa Road) itafungwa kuanzia chuo
cha DUCE hadi msikitini kuanzia saa 4 asubuhi.
Magari
maalumu yenye sticker pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani. Vilevile
washabiki wanakumbushwa kuwa hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha au
vifaa vyovyote vya chuma.
No comments:
Post a Comment