Klabu
ya Barcelona ikikabiliwa na Mashitaka Kortini kwa kukwepa kulipa Kodi
halali za Nchini Spain wakati wa Uhamisho wa Neymar kutoka Santos, Klabu
ya Barcelona imelipa nyongeza ya Kodi ya Euro Milioni 13.6 kwenye Dili
ya Staa huyo wa Brazil.
Licha ya kupinga kuwa ilifanya mbinu kukwepa ulipaji Kodi, Barcelona wamekubali kulipa Nyongeza ya Kodi ya €13,550,830.56 na wao kudai wamefanya hivyo ili kukidhi madai ya ziada na pia kusafisha Jina la Klabu yao.
Mbali ya Kesi ya Ukwepaji Kodi, Barcelona pia inachunguzwa na Mahakama hiyo hiyo huko Spain kwa Ubadhirifu wa Fedha kufuatia Uhamisho wa Neymar madai ambayo yalipelekwa Kortini na Mwanachama wa Barcelona, Jordi Cases.
Madai haya ndio yalimfanya Rais wa Barcelona, Sandro Rosell, ajiuzulu wadhifa wake na nafasi yake kuchukuliwa na Makamu wake Josep Bartomeu ambae alipasua kuwa gharama waliyoipata Barca kwa kumnunua Neymar ni Euro Milioni 90 na si Euro Milioni 57.1 zilizotangazwa awali.
Sakata hili pia limeibua hisia kali huko Brazil ambapo Klabu ya Santos imedai wao walilipwa Euro Milioni 17 tu na Fedha nyingine zote kwenda kwa Familia ya Neymar na Wawakilishi wake wengine.
Pia, wapo Wamilikiji wengine wa Haki za Neymar ambao wametishia kwenda Mahakamani huko Brazil kudai Mgao wao kwenye Mauzo ya Neymar.
Neymar alihamia Barcelona mwanzoni mwa Msimu huu.

No comments:
Post a Comment