BONDIA Alex
Michael wa klabu ya JKT Mgulani anayepigana kwenye uzani wa kg 60 amekuwa
bondia bora wa mashindano ya ngumi mkoa wa Dar es Salaam yaliyokuwa yakifanyika
katika Ukumbi wa Panandi, Ilala Bungoni.
Mashindano
hayo ambayo yalianza Januari, 27 yalimalizika juzi kwa jumla ya mapambano 48
kuchezwa ikiwepo ya wanawake na watoto.
Akizungumza
baada ya mashindano hayo kumalizika, Mwenyekiti wa Chama cha ngumi za Ridhaa,
mkoa wa Dar es Salaam, (DABA) Karoly Godfrey, alisema kuwa mashindano hayo
yalimefana na yamesaidia kujua na kujionea vipaji vingi katika mkoa wa Dar es
Salaam.
“Lengo la
mashindano limefanikiwa kwani mabondia wengi wameshikiriki kwa sababu mkoa wa
Dar es Salaam una takribani miaka mitatu bila kuandaa mashindano ya ngumi na
haya ni mashindano ya kwanza kwa uongozi wetu kuandaa tangu tuingie madarakani
mwaka jana”, alisema Godfrey
Pia alisema
wana changamoto za vifaa hali inayofanya kuchelewesha muda wa mchezo kusubiri
mabondia kubadilishana hivyo wanaomba wadau kuwasaidia ili kuinua mchezo huo.
Katika
mchezo wa fainali uzito wa kg 49, bondia Mussa Mchomamnga alishinda baada ya mwamuzi kumwokoa bondia Antony Idoa
kutokana na kuzidiwa na bondia Hafidh
Bamtula alishinda kwa pointi mbili kwa moja dhidi ya bondia George Constatino
hali iliyozua malalamiko kwa mmoja wa jaji wa mchezo huo alikuwepo baba mzazi
wa Hafidh Bamtula.
Kwenye uzito
wa kg 56 bondia Emilian Patrick alishinda kwa pointi mbili kwa moja dhidi ya
bondia Frank Nicholaus, mchezo ambao uliwazutia wengi kutokana na ufundi wa
kurushiana ngumi kwa zamu.
Bondia Alex
Michael alishinda kwa pointi Yousole Said kwenye pambano la uzito wa kg 60 na
Victor Njaiti alishinda kwa pointi dhidi ya Haruna Husein kwenye pambano la
uzito wa kg 64.
Naye bondia
Mohamed Chibumbui alimpiga Abdul Ashid kwa pointi mbili kwa moja kwenye pambano
la kg 69, huku Hamad Halfan akimpiga kwa KO bondia Salum Jafari kwenye pambano
la kg 75.
Naye
mwanadada Ellen Mushi alimpiga Siwatu Kimbe kwa pointi mbili kwa moja kwenye
pambano la raundi nne huku Sarah Andrew akimpiga Grace Michael kwa pointi
kwenye pambano la raundi nne pia.
No comments:
Post a Comment