Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 14, 2014

YANGA KUIVAA ALTAY SK LEO


Yanga wakijifua Uturuki jana, picha na Baraka Kizguto, Ofisa Habari wa Yanga SC

Na Baraka Kizuguto, Antalya
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara na vinara wa ligi hiyo msimu huu, Yanga SC ya Dar es Salaam itashuka dimbani leo Jumatano kucheza mchezo wa pili wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Altay S.K iliyopo Ligi Daraja la Pili nchini Uturuki.
Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi hiyo jana asubuhi na jioni katika viwanja vya hoteli ya Sueno Beach Side kujiandaa na mchezo huo wa Jumatao ambao ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kaimu kocha mkuu, Charles Boniface Mkwasa amesema anashukuru vijana wake wote wanaendelea vizuri katika kambi ya mafunzo, hakuna mchezaji ambaye amekosa mazoezi hata siku moja na hali ya hewa inaruhusu kabisa kufanya mazoezi, hivyo vijana wanaitumia ipasavyo nafasi hiyo.
Akiongelea mchezo wa jumatano(leo), Mkwasa amesema anawaandaa vijana kuendelea kufanya vizuri katika mchezo huo na ataendelea kutoa nafasi kwa kila mchezaji aliyekuja nchini Uturuki apate nafasi ya kucheza kwani kupata nafasi ya kucheza michezo ya kirafiki huku ni njia ya kuwakomaza na kuweza kujiamani katika mechi kubwa za mashindano.
Jana Yanga ilifanya mazoezi mara moja tu asubuhi kujiandaa na mchezo huo wa Jumatano dhidi ya timu ya Altay SK ambayo pia inajiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Daraja Pili nchini Uturuki.

Mara baada ya mchezo huo wa Jumatano, Yanga itakamilisha ziara yake ya mafunzo wiki ijayo kwa kucheza na timu ya Simurq Zaqatala FC ya nchini Azberbaijan iliyopo katika Ligi Kuu ya nchi hiyo na msimu uliopita ikiwa imekamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ya Azerbaijan

No comments:

Post a Comment