Stanislas Wawrinka raia wa Uswis amefanikiwa kutwaa taji la michuano ya wazi ya Australia kwa kumchapa Mhispania Rafael Nadal katika mchezo wa fainali.
Wawrinka alimfunga Nadal aliyekuwa akisumbuliwa
na matatizo ya mgongo kwa seti tatu kwa moja, ikiwa ni kwa matokeo ya
6-3 6-2 3-6 6-3.
Anakuwa raia wa pili wa Uswis kunyakuwa taji la Grand Slam kwa upande wa wanaume kwa mchezo wa tenesi wa mchezaji mmoja mmoja.
Pia ni mtu wa pili kunyakuwa taji kubwa kama
hilo akiwa ametoka nje ya vinara wanne wa juu wa dunia wa mchezo wa
tenesi, baada ya Juan Martin Del Potro kufanya hivyo kwenye michuano ya
US Open mwaka 2009.
Nadal ambaye awali alisema kusumbuliwa na
matatizo ya mgongo lakini hakujitoa kwenye michuano hiyo ambayo imefikia
tamati huko Melbourne Park.
" Sikupenda kusema kwamba sitocheza mchezo wa
fainali, ni jambo ambalo nachukia sana hata kama niligundua kuwa nina
maumivu ya majeraha" Alisema Nadala mwenye umri wa miaka 27.
" Huu sio wakati wa kuzungumzia maumivu
niliyoyapata, ila ni wakati wa kumpongeza Stan. Amecheza vizuri sana na
ukweli anastahili taji hili.
Ni mtu mwema, mtu mzuri na rafiki yangu, nina furaha sana kwake kuwa bingwa" Alisema Nadal.
Naye Wawrinka alimsifu Nadal kwa kuwa bingwa wa
kweli na kinara wa kweli wa tenesi duniani kwa wanaume, alikiri
hujisikia furaha kupambana na kumshinda bingwa kama Nadal.
Wawrinka hajawahi kushinda hata seti moja katika
michezo yote 12 aliyokutana na Nadal huko nyuma, na alicheza fainal
yake ya kwanza akiwa kwenye nafasi ya 19 ya ubora wa tenesi duniani.
No comments:
Post a Comment