Leo timu za taifa za Ghana na Libya zitakuwa zikishuka dimbani kusaka
nafasi ya kucheza hatua ya mtoano ya fainali za mataifa ya Afrika ya CAF
watakapokuwa wakishuka katika dimba la Free State Stadium.
Mataifa yote hayo mawili yalishinda katika michezo yao ya ufunguzi Jumatatu usiku mjini Bloemfontein.
Ushindi kwa yoyote baina yao itakuwa unawapa nafasi ya kusonga mbele
katika robo fainali ya michuano hiyo na la muhimu zaidi kumaliza katika
nafasi ya juu katika kundi C.
Mshindi wa kwanza wa kundi hili atakutana dhidi ya mshindi wa nafasi ya
pili wa kundi D, kundi ambalo linaonekana kama mchekea katika michuano
hiyo.
No comments:
Post a Comment