Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 14, 2014

ARSENAL ILIPOIPIGA ASTON VILLA 2-1 NA KURUDI KILELENI

Olivier Giroud (kushoto) akishangilia bao lake
Jack Wilshere 34' • Olivier Giroud 35 
Kipindi cha kwanza kimewaendea vyema Arsenal wakiwa ugenini Villa Park kucheza na wenyeji Aston Villa baada ya kuichapa bao mbili za haraka katika dakika ya 34 Jack Wilshere ameifunga bao la kwanza na baadae baada ya dakika moja kupita Oliver Giround akamaliza biashara kwa kufunga bao jingine katika dakika ya 35. Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Arsenal wameenda mapumziko wakiwa juu ya bao 2-0 dhidi ya wenyeji Aston Villa.
Kipindi cha pili dakika ya 76 Christian Benteke akatupia bao kwa kichwa baada ya kupata mpira uliopigwa kutoka kati na kuwapita mabeki wa Arsenal na kumfunga kipa wa Gunners na kufanya mtanange kuwa 2-1. Ushindi huu wa Arsenal unawarudisha kileleni wakiwa na pointi 48 huku Aston Villa wakibaki pale pale katika nafasi ya 11 wakiwa na pointi 23.Benteke leo kazinduka na kutupia bao na hapa alikuwa akishangilia bao hilo la pekee kwa timu yake na likiwa la kwanza kwake kwenye mitanange 12 iliypigwa. Olivier Giroud akifunga bao la pili ndani ya dakika moja baada ya Jack kufunga la kwanza.
 Giroud akishangilia bao lake na kupongezwa na wenzie hapa..
Kocha wa Aston Villa Paul Lambert akishangaa bao hizo mbili za shapu shapu kwenye uwanja wao Villa Park
Nathan Baker aliumia na hapa alikuwa akipewa huduma ya haraka uwanja..pamoja na hayo hakuweza kuendelea na mchezo huo ameondolewa na kwenda kutibiwa   Christian Benteke akiziona nyavu kipindi cha pili dakika ya 76
Benteke akishangilia bao lake la kwanza na la pekee katika mechi 12 zilizopita
 Mchezaji wa Villa Nathan Baker aliumia baada ya Serge Gnabry kuachia shuti kali ndani ya box
  Baker katika taswira ya janga lililompata  Nathan Baker akipata matibabu ya haraka uwanjani baada ya kubamizwa na shuti la Gnabry  Mapema viongozi wote wa timu mbili wakisalimiana kabla ya mtanange kuanza live Villa Park kushoto ni Paul Lambert kulia ni Arsene Wenger.

No comments:

Post a Comment