Main man: Robert Lewandowski (kushoto) anaweza kuondoka Borussia Dortmund na kujiunga na Bayern Munich |
Zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya kufika mwezi Januari ambao kimsingi dirisha dogo la usajili litakuwa likifunguliwa.
Hebu
tuangazie kwa pamoja tupate kujua wachezaji nyota kumi barani Ulaya
ambao watakuwa nje ya mikataba wakati wa kiangazi na akina nani ambao
watakuwa wako tayari kukatisha viporo vya mikataba yao kwa makubaliano
ya fidia.
Robert Lewandowski
Mshambuliaji mwenye umri w miaka 25 wa Borussia Dortmund
Mshambuliaji
huyu raia wa Poland ni mmoja kati ya kifaa cha nguvu katika soka,
anatarajiwa kuweka wazi nini mipango yake ya baadaye mwezi Januari
utakapo wadia.
Inaarifiwa
kuwa Bayern Munich ndio eneo ambalo hasa mshambuliaji ataelekea lakini
usiache kuvitazama vilabu kadhaa vya Barclays Premier League ambavyo
vinapiga hatua kuelekea kupata huduma yake.
Arsenal, Chelsea na Manchester United vyote vimeonyesha nia huku Real Madrid pia inaonekana kumnyemelea.
Xabi Alonzo kiungo wa Reala Madrid mwenye umri wa miaka 32
Kiungo
huyo wa zamani wa Liverpool kuna taarifa kuwa huenda karejea katika
klabu yake ya zamani, ingawa kuna taarifa ya watu wenye majina nchini
humo kugomea hilo nchini Hispania.
Mashabiki wa Real Mdrid wanataka aendelee kusalia na katika
kulithibitisha hilo wamekuwa wakimuunga mkono katika michezo ya hivi
karibuni. Pia kuna taarifa nchini Hispania kuwa Jose Mourinho huenda
akamchukua na kujiunga na Chelsea.
Maestro: Xabi Alonso
Andrea Pirlo mwenye miaka 34, kiungo Juventus
Ni
zaidi ya habari kuwa Pirlo, mmoja kati ya wachezaji wenye heshima kubwa
mchezoni atasaini mkataba wa kuongeza muda ndani ya klabu yake ya
Juventus mwezi January.
Klabu hiyo ya nchini Italia haina wasiwasi na juu ya mpango huo mpya kwa Pirlo na kwamba litakuwa ni jambo bora.
Hata
bado anaendelea kufukuziwa na vilabu mbalimbali Ulaya na hilo ni
jaribio kubwa na swali kubwa ni nini kitatokea mwezi Januari.
Kiungo wa Italia na Juventus maestro Andrea Pirlo (kulia) akipambana na mchezaji wa Fiorentina Borja Valero
Bafetimbi Gomis umri wa miaka 28 Lyon
Swali ni je mshambuliaji huyu mfaransa ataondoka na kuelekea kucheza soka nchini England?
Wakala
wake anasema huko hasa ndiko anakokutana kuelekea. Newcastle tayari
wameonyesha nia kwake. Ilikuwa kidogo wafanikiwe kumsajili wakati wa
majira ya kiangazi lakini ilishindikana kutokana na kutokukubaliana juu
ya suala la mshahara.
Cardiff na Swansea pia wanapiga hatua kumnasa
Mshambuliaji mfaransa Bafetimbi Gomis anataka kuondoka Lyon
Jeremy Menez , 26, Paris Saint- Germain
Uwezekano
wa mshambuliaji huyo wa kifaransa kuondoka linaonekana kama ni jambo
jepesi kwa vilabu kadhaa vya Ulaya na wengi wakionyesha nia. Amekuwa
akihusishwa na kutaka kuelekea Liverpool, lakini huenda wakakutana na
upinzani kutoka katika vilabu vya Inter Milan, Roma na Juventus.
Anaonekana kama anataka kuondoka ingawa pia wanaonekana wanapata
kumuongezea mkataba.
Jeremy Menez huenda akaongeza mkatabat Paris Saint-Germain
Victor Valdes ,31,mlinda mlango wa Barcelona
Mlinda
mlango huyu amekuwa nje kwa kipindi cha karibu wiki sita akisumbuliwa
na misuli na klabu yake ya Barcelona siku zinakwenda harijojo. Paris
Saint-Germain inamtaka huku taarifa nyingine nchini Hispania zikiarifu
kuwa Manchester City wako na mpango wa kumnasa. Hizo zinaweza zikawa ni
taarifa mbaya kwa mlinda mlango namba moja wa England No 1 Joe Hart.
Victor Valdes
Diego,28, kiungo wa Wolfsburg.
Kiungo
huyu mshambuliaji wa Ki-Brazil anakaribia kuondoka katika kikosi cha
Wolfs kinachoshiriki ligi ya Ujerumani Bundesliga. Anataka kuelekea
Premier League na amekuwa akieleza wazi kuwa anaipenda Arsenal au
Southampton. Aina yake ya uchezaji inaonekana kufanana na pande zote
mbili hizi ingawa bado vilabu hivyo havija onyesha wazi kuanza
kumfuatilia.
Diego
Esteban Cambiasso, 33, kiungo wa Inter Milan
Huyu
pia ni mchezaji mwenye umri wa kutosha ambaye ana mchango mkubwa katika
kiungo na anaweza kuongeza uzoefu wake wa dimba la kati katika klabu
yoyote ile duniani.
Inter
inaarifiwa kuwa inamhitaji kuendelea kuwa naye, lakini suala la yeye
kutaka kurejea nyumba ni linaonekana sio swali gumu tena kupatiwa
majibu.
Esteban Cambiasso
Urby Emanuelson,27, kiungo wa AC Milan
Tayari
ana uzoefu wa kutosha katika ligi kuu ya England wakiti akiwa na klabu
ya Fulham kwa mkopo, ambako bosi wake wa zamani Martin Jol alichukizwa
alipoona akiondoka kwa muda mfupi Kiungo huyu M-Dutch alikaririwa
akisema anataka kucheza tena.
Urby Emanuelson
Wachezaji wa Primier League watakao kuwa nje ya mkataba majira ya kiangazi hawa chini
Nemanja
Vidic, Samuel Eto’o, Bacary Sagna, Younes Kaboul, Patrice Evra, John
Terry, Joleon Lescott, Ashley Cole, Frank Lampard, Rio Ferdinand
Blaise Matuidi, 26, kiungo wa PSG
Blaise Matuidi, 26, kiungo wa PSG
Kuna
tetesi kwamba Chelsea na Manchester City wanapanga miopango ya kuandaa
'pre-contract
offers' kwa ajili ya Matuidi endapo itashindikana kukubaliana na
masharti mapya na PSG. Kiungo huyo ana njia nyeupe ya kuelekea Premier
League, lakini anasubiri kile ambacho kitawekwa mezani na klabu yake ya
sasa.
Kajichokea: Blaise Matuidi huenda akaondoka PSG kama masharti mapya ya mkataba yatashindikana.
No comments:
Post a Comment