Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 2, 2013

ENGLISH PREMIER LEAGUE: HULL CITY 3 vs LIVERPOOL 1, MAJOGOO YACHINJWA UGENINI


HULL CITY 3 v LIVERPOOL 1
Hull City, wakiwa kwao KC Stadimu, leo wamepata ushindi wao wa kwanza kabisa dhidi ya Liverpool walipoifunga Bao 3-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England. 
Hull City, chini ya Meneja Steve Bruce ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man United, walitangulia kufunga baada ya shuti la Jack Livermore kumbabatiza Beki wa Liverpool Martin Skrtel na kutinga wavuni.
Frikiki ya Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, iliwapa Liverpool Bao la kusawazisha kabla Haftaimu.

Kipindi cha Pili, ulinzi hafifu wa Liverpool uliwapa mwanya Hull City kupachika Bao la Pili Mfungaji akiwa David Meyler
Bao la Tatu la Hull City ni la kujifunga mwenyewe Martin Skrtel kwa kichwa.
Kipigo hiki kimewaacha Liverpool wabaki Pointi 7 nyuma ya Vinara Arsenal na wapo hatarini kupokonywa Nafasi ya Pili na Chelsea ambao wanacheza Mechi yao hii leo. 
Jake Livermore akiachia shuti kali na kuipatia bao timu yakeUshindi mtamu.....hapa akipeta baada ya kufunga bao!! Liverpool Hoi!!!Pongezi: Wachezaji wakipongezana!

Steven Gerrard  akinyoosha mpira kwa frii kiki na kufunga bao dakika ya 27..Furaha baada ya Steven Gerrard  kufunga bao hapaKipa Allan McGregor hoi!!Bao la zawadi kwa Hull City 
Wachezaji wa Hull City wakishagilia bao la tatu na la ushindi kwao 
Vichwa chini..

No comments:

Post a Comment