Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya marekebisho ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ili kupisha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania na Msumbiji.
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza kwa mashindano ya wanawake wenye
umri chini ya miaka 20 itachezwa Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu) Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.
U20
tayari imehamishia kambi yake hosteli ya Msimbazi Center, Dar es Salaam
kutoka JKT Ruvu mkoani Pwani tangu wiki iliyopita kujiandaa kwa mechi
hiyo. Fainali za Kombe la Dunia kwa U20 wanawake zitafanyika mwakani
nchini Canada.
Marekebisho
ya ratiba ya VPL yamegusa raundi zote tatu zilizobaki kukamilisha
mzunguko wa kwanza. Kutokana na marekebisho hayo mechi za raundi ya 11
zitakuwa ifuatavyo; Oktoba 28 mwaka huu ni Coastal Union vs Mtibwa
Sugar, Oljoro JKT vs Ashanti United, Ruvu Shooting vs Kagera Sugar na
Simba vs Azam. Oktoba 29 mwaka huu ni Tanzania Prisons vs Mbeya City,
Yanga vs Mgambo Shooting na Rhino Rangers vs JKT Ruvu.
Raundi
ya 12 ni kama ifuatavyo; Oktoba 31 mwaka huu ni Simba vs Kagera Sugar,
Novemba 1 mwaka huu ni JKT Ruvu vs Yanga. Novemba 2 mwaka huu ni Mgambo
Shooting vs Coastal Union, Tanzania Prisons vs Oljoro JKT, Azam vs Ruvu
Shooting, Mtibwa Sugar vs Rhino Rangers na Mbeya City vs Ashanti United.
Raundi
ya 13 ni kama ifuatavyo; Novemba 6 mwaka huu ni JKT Ruvu vs Coastal
Union, Ashanti United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino
Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar. Novemba 7
mwaka huu ni Azam vs Mbeya City.
Mechi
za kufunga raundi ya 10 zitachezwa keshokutwa (Oktoba 23 mwaka huu)
kama ratiba inayoonesha. Mechi hizo ni kati ya Coastal Union vs Simba,
Tanzania Prisons vs Kagera Sugar na Yanga vs Rhino Rangers.
No comments:
Post a Comment