Chama
cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DBU) kimetuma maombi ya Hati ya
Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wawili wa Tanzania ili
wajiunge na klabu mbili tofauti za nchini humo.
Maombi
hayo yaliyotumwa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni kwa
ajili ya wachezaji Henry Claud Egito aliyezaliwa Desemba 31, 1984
jijini Dar es Salaam, na Dominic Johnson aliyezaliwa Agosti 14, 1991
jijini Tanga.
Wachezaji
hao wanaombewa ITC kama wachezaji wa ridhaa. Egito anaombewa hati hiyo
ili ajiunge na klabu ya FSV Lokomotive Dresden wakati Johnson anatakiwa
na klabu na TSV 1967 Schwabbruck.
No comments:
Post a Comment