Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, September 18, 2013

UEFA CHAMPIONS LEAGUE:RATIBA VIWANJA 8 KUWAKA MOTO TENA LEO JUMATANO - BARCELONA v AFC AJAX, AC MILAN v CELTIC FC, CHELSEA v fc BASEL 1893...


BARCELONA na AJAX ni Klabu kubwa na zenye Historia iliyotukuka Barani Ulaya, huku zote zikiwa zimetwaa Ubingwa wa Ulaya mara 4 kila mmoja, lakini cha ajabu ni kuwa Klabu hizi hazijawahi kukutana na Jumatano hii Mechi ya Kundi H la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, itakayochezwa Nou Camp itakuwa Mechi yao ya kwanza kabisa.

Huko Nou Camp, Wadau wake daima hawataisahau Ajax kwani kuiiga kwao ndio kumezaa mafanikio makubwa kwa Barca katika Miongo mitatu iliyopita.
Ilikuwa Mwaka 1992 wakati Barca walipotwaa Ubingwa wao wa Ulaya kwa mara ya kwanza na wakati huo Meneja wao alikuwa Johan Cruyff ambae ndie alieiongoza Ajax kutwaa Ubingwa huo mara 3 akiwa Mchezaji wao.
BARCELONA na AJAX ni Klabu kubwa na zenye Historia iliyotukuka Barani Ulaya, huku zote zikiwa zimetwaa Ubingwa wa Ulaya mara 4 kila mmoja, lakini cha ajabu ni kuwa Klabu hizi hazijawahi kukutana na Jumatano hii Mechi ya Kundi H la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, itakayochezwa Nou Camp itakuwa Mechi yao ya kwanza kabisa.Barcelona
Cruyff ndie alieuleta Mfumo wa 4-3-3 Barca na staili yao ya uchezaji ya sasa kuendelezwa na aliekuwa Mwanafunzi wa Cruyff, Pep Guardiola.
Kwa sasa Johan Cruyff ni Mshauri wa Ajax lakini hiyo Jumatano hatakanyaga Nou Camp kwa vile ana bifu na Rais wa Barca, Sandro Rosell.
Msimu huu, Barca hawajaanza kwa kishindo lakini wameshinda Mechi zao zote 4 za La Liga na pia kutwaa Super Cup ya Spain.
Jumamosi walihitaji Bao la Dakika za Majeruhi la Alexis Sanchez kuifunga Sevilla Bao 3-2 baada ya kubwaga uongozi wa Bao 2-0 katika Dakika 10 za mwisho.
Msimu huu, Barca wapo chini ya Kocha mpya Gerardo ‘Tata’ Martino na kwa sasa Klabu ina matatizo ya Difensi huku Beki wa kushoto Jordi Alba akiwa nje kwa Wiki 3 kutokana na matatizo ya Musuli za Pajani na Nahodha Carles Puyol bado hayuko fiti baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye Goti Niezi kadhaa iliyopita ingawa ameanza Mazoezi.
Kwa upande wa Ajax, ambao Jumamosi kwenye Ligi yao waliifunga 2-1 PEC Zwolle,  Kocha Frank de Boer, ambae aliwahi kuichezea Barca, anacho Kikosi kamili fiti akiwemo Fowadi Bojan Krkic ambae yuko Ajax kwa Mkopo kutoka Barca lakini yuko huru kuicheza Mechi hii.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
RATIBA:MATOKEO
[Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku]
Jumanne 17 Sep 2013
Manchester United FC 4 v 2 Bayer 04 Leverkusen
Real Sociedad de Fútbol 0 v 2 FC Shakhtar Donetsk
Galatasaray A.Ş. 1 v 6 Real Madrid CF
FC København 1 v 1 Juventus
SL Benfica 2 v 0 RSC Anderlecht
Olympiacos FC1 v 4 Paris Saint-Germain
FC Bayern München 3 v 0 PFC CSKA Moscow
FC Viktoria Plzeň 0 v 3 Manchester City FC

RATIBA: 
[Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku]
Jumatano 18 Sep 2013
FC Schalke 04 v FC Steaua Bucureşti
Chelsea FC v FC Basel 1893
Olympique de Marseille v Arsenal FC
SSC Napoli v Borussia Dortmund
FK Austria Wien v FC Porto
Club Atlético de Madrid v Football Club Zenit
AC Milan v Celtic FC
FC Barcelona v AFC Ajax

No comments:

Post a Comment