Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima |
Egino Chusi akicheza gofu kwenye fainali za Lugalo |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima akimkabdi Abdallah Yusuph |
MCHEZAJI Athuman Chiundu ameibuka bingwa wa mashindano ya
gofu ya kombe la CDF yaliyoandaliwa na klabu ya Lugalo na kudhaminiwa na
kinywaji cha Konyagi.
Abdala katika siku ya kwanza alipiga gofu 71 na siku ya pili
alipiga 70 na kumaliza akiwa amefikisha 141 na kumfanya kuwa bingwa na
kuzawadiwa kikombe pamoja na jokofu dogo.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Abdallah Yusuph ambaye alipiga
gofu 151 na kupata kombe na pamoja na macrowaves.
Kwa upande wa wanawake Vicky Elias alishika nafasi ya pili
na kufanikiwa kupata kombe na rice cooker huku nafasi ya kwanza ikienda kwa Hitech
Valambia.
Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo mgeni rasmi
ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job
Masima, alisema anashukuru kwa udhamnini wa kinywaji cha konyagi kwani imepanua
wigo wa wachezaji kuongezeka.
“Nashukuru Konyagi kwa udhamini wao kwani umesaidia kuongeza
idadi ya washiriki hadi kufikia 72 kwa mwaka huu”, alisema Masima
Mashindano hayo ambayo ni mara ya nne yakichezwa yalianza
kutimua vumbi Septemba 7 na kumalizika Septemba 8 na yalishirikisha wachezaji
maarufu kama Gidioni Sayore, GM Waitara, na Victor Kimesera
No comments:
Post a Comment