LONDON, England
LIGI Kuu
England ilianza rasmi mwisho wa wiki hii, ambapo ilishuhudiwa vigogo mbalimbali
vikiumana ili kusaka pointi tatu muhimu.
Mara baada
ya vigogo hivyo kuchuana vikali, tayari imeshaonekana kwamba wataweza kutikisa
kwenye michuano hiyo.
Kutokana na uwezo
waliouonesha wachezaji hao, wachambuzi wa masuala ya soka nchini England
wamejaribu kuangalia kikosi cha wiki kinachoundwa na nyota waliotikisa katika
siku ya kwanza ya michuano hiyo.
Wanasema Gabriel
Agbonlahor ambaye
kwa sasa ana umri wa miaka 26 na ambaye alisajiliwa msimu uliopita, alikuwa
mwiba kwa Arsenal katika mechi hiyo ya Jumamosi.
Wanasema Christian
Benteke alikuwa msaada mkubwa kwa Aston Villa,
lakini mapande ambayo alikuwa akitengewa na Agbonlahor ndiyo yaliyomfanya aonekane kuwa
tishio.
Mbali na
mchezaji huyo, wachezaji wengine watatu ambao walionekana watakuwa tishio ni
pamoja na Ross Barkley.
Wanasema kuwa hata wachezaji wenzake wa
zamani, Martin Keown na Jamie Carragher vilevile wanamzimia.
Wanasema kwa
sasa siri ipo wazi, kiungo huyo wa Everton mwenye umri wa miaka 19, alionesha kila kitu kwenye mchezo dhidi ya
Norwich, likiwamo bao tamu alilofunga.
Wachambuzi
hao wanasema mchezaji huyo anaonekana kuwa na kiwango kama alichokuwa
nacho wachezaji, Paul Gascoigne na Steven Gerrard.
Wanasema nyota
huyo ana uwezo wa kusimama vyema kwenye nafasi ya kiungo.
2) V ni kwa
maana ya Victor
Victor
Wanyama ni Mkenya ambaye ametokea katika timu ya Celtic, ambaye naye alifanya
vizuri kwenye mechi ambayo timu yake iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya West Bromwich.
Kuonekana
kwake uwanjani ina maana kwamba kwa sasa kuna wachezaji 100 wa kigeni
wanaokipiga Ligi Kuu ya England.
Idadi hiyo imefikiwa
ikiwa ni baada ya wiki ya kwanza ya miaka 1992, kuwepo wachezaji nane kutoka mataifa ya
kigeni, lakini kwa sasa ligi hiyo
imekuwa ni ya mataifa mbalimbali.
3) Mata
Kevin de
Bruyne anaonekana atakuwa mchezaji ambaye ataleta msisimko kwenye kikosi
cha Chelsea.
Hata hivyo
timu haiwezi kukamilika bila kuwepo, Juan Mata.
Mchambuzi
huyo wa masuala ya soka anasema kuwa kinara huyo ambaye ni mchezaji bora wa
mwaka msimu uliopita Chelsea ndiye
chaguo lake na kwamba wachambuzi hao wanasema watafurahi kuona kocha Jose
Mourinho akimtumia vilivyo.
Kwa upande
wa Manchester United, kocha wa timu hiyo, David Moyes, kwanza alimuacha nje ya kikosi
chake, Wilfried Zaha na kuwachezesha
wachezaji ambao aliamini wangeweza kuwa na nidhamu na kucheza vizuri.
Lakini hata
hivyo, kwa zaidi ya dakika 30 timu yake iliutafuta mpira kwa tochi kabla ya
umaliziaji kati ya RVP na Danny Welbeck kuleta kitu tofauti kwa Swansea.
Mwingine
aliyetakata alikuwa ni Tom Hitchcock, ambaye alimfurahisha baba yake kipa wa makocha
kwenye timu ya QPR, Kevin.
Katika
mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Loftus, Tom alifunga bao dakika ya 90 lililoipa ushindi dhidi ya Ipswich, ikiwa ni muda mfupi akitokea benchi.
“Nilifunga
bao kwenye michuanoya Kombe la FA wakati nikicheza na baba lakini siyo kwenye Ligi Kuu,” alikaririwa
akisema mchezaji huyo.
Alisema kuwa
kutokana na hali hiyo, anaweza kufunga mabao mengi ya ushindi wakati baba yake
anapokuwa upande wake.
Kwa
upande wake Kevin Nolan, ambaye
alipachika bao lililoipa ushindi West
Ham dhidi ya Cardiff, naye anatajwa
kutakata kutokana na pasi 16 alizowapa Mark
Noble, Joe Cole na Stewart Downing.
Hata hivyo,
inaelezwa kuwa nahodha huyo wa Hammers anatahadharishwa kuwa makini kutokana na
kwamba mabao mengi aliyopoteza yanaweza kuifanya timu ikaanza kufanya vibaya.
Nolan anatajwa kuwa nguzo muhimu kwa kocha, Sam Allardyce na bao lake kama hilo ndilo
lilimfanya kuingia kwenye orodha ya viungo sita bora wanaofunga mabao kwenye
histori ya Ligi Kuu ya England.
.Timu ya
wiki iliyopendekezwa na wachambuzi hao
ambayo inaweza kutumia mtindo wa
(4-3-3) ni Mignolet (Liverpool); Whittaker (Norwich),
Vidic (Manchester United), Lovren (Southampton), Shaw (Southampton); Delph
(Aston Villa), Wanyama (Southampton), Barkley (Everton); Agbonlahor (Aston
Villa), Van Persie (Manchester United), Welbeck (Manchester United).
Viungo
wanaoongoza kwa ufungaji mabao hadi sasa ni
Frank
Lampard- 166
Ryan Giggs 109
Paul Scholes 107
Steven
Gerrard 98
Gary Speed 80
Kevin Nola 62
Robert Pires 62
David
Beckham 62
No comments:
Post a Comment