Cardiff City wameifunga timu ya
Manchester City bao 3-2 leo kwenye ligi kuu England, Kipindi cha kwanza
kilimalizika bila kufungana kati Cardiff City iliyopanda daraja msimu
huu na Manchester City, Kipindi
cha Pili Manchester City walianza mtanange kwa kujiamini na kuweza
kujuwa wapi walikuwa wanakosea kipindi cha kwanza, Dakika ya 52 Dzeko
akipewa basi safi na kuachia shuti kali ambalo limewapita mabeki na kipa
wao Cardiff na kuishilia nyavuni. Nao Cardiff City wakaongeza bidii ili
kusawazisha bao hilo dakika ya 50 mchezaji Aron Gunnarsson akaisawazishia bao na kufanya 1-1.baada ya piga nikupe ya shabulizi lao moja hilo la kipindi cha pili. Dakika ya 79 mchezaji Fraizer
Campbell aliyekokosa kosa mabao kadhaa kipindi cha kwanza akafanikiwa
kuwapachikia bao la pili Cardiff City baada ya kona safi kupingwa na Fraizer Campbell akaingia nao mpira kwa kuupiga kichwa hadi nyavuni. Mashabiki wa Cardiff City wakaanza kuwazomea City kwa kuanza kuwaiga jinsi ambavyo mashabiki wa City wanavyoshangilia. Haikupita muda mrefu Cardiff City wakapata bao jingine la tatu na kufanya 3-1 dhidi ya City likipachikwa na yule yule mwiba wao Fraizer Campbell katika dakika ya 87. Dakika za lala salama City wakapata bao la pili na kufanya 3-2 bao hilo pa pili likifungwa na Álvaro Negredo dakika ya 90+2'
na mpira ukaisha City wakiwa wanakumbuka shuka wakati kumekucha!!
Ushindi huu unawapandisha Cardiff City nafasi ya 11 wakitoka kwenye
mstari mwekundu. Mmiliki
wa Cardiff Vincent Tan (katikati) nae alikuwa mmoja wa watazamaji hapa
jioni hii kwenye uwanja wa Cardiff City Stadium
Campbell akishangilia baada ya kutupia bao!!
Mchezaji wa Cardiff Gary Medel akichuana hapa na Fernandinho
Aron Gunnarsson akisawazisha bao!!
Sergio Aguerona machungu ya kufungwa hapa!!
Edin Dzeko akifunga bao hapa kwa shuti kali
Fraizer Campbell kwenye patashika na kipa wa City Joe Hart
Alvaro Negredo akikata tamaa baada ya muda kuwatupa mkono!!!
No comments:
Post a Comment