RAIS
wa Real Madrid, Florentino Perez, kwa mara nyingine amesema kwamba hataki
kabisa kumuuza Cristiano Ronaldo, ambaye bado anahusishwa na kutua Manchester
United na PSG.
Perez
alifafanua: "Nitafanya kila liwezekanalo kwa nguvu zangu ili kumpa mkataba
mpya. Amebakiza miaka miwili katika mkataba wake, ni mchezaji bora duniani na
ataiboresha timu yetu, yeye ni kama kiongozi.
"Sitamuuza
hata kwa Euro milioni 1,000, hii si klabu ya kufanya mauzo. Ningependa awepo
hapa hadi atakapotundika daluga, itakuwa ni vema kabisa."
No comments:
Post a Comment