Staa wa
Bongo Movie ambaye pia ni mmilikiwa kampuni ya Endless film Wema Sepetu
amemfikisha mama yake mzazi anayejulikana kama Miriam Sepetu kwenye Kituo cha
Polisi Kijitonyama jijini Dar es salaam kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na
kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani nadani ya nyumba yake.
Tukio hilo
lilitokea usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama,
jijini Dar.
Mbali na
mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye
Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni
mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.
“Wema
alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza kumchapa
makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na
kumtia hasara staa huyo,”
Haikujulikana
mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa
ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.
Wema
alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye
kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.
No comments:
Post a Comment