Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 31, 2013

NSSF QUEENS YAIADHIBU ZSSF QUEENS 35-29 BONANZA LA PASAKA


 Kikosi cha ZSSF Queens kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na NSSF Queens katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana mjini Zanzibar.  (Picha na  Habari Mseto Blog)
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (SMZ), mama Asha Seif Idd akifungua mashindano ya tamasha la Pasaka kwa timu za netiboli yaliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar na kuzikutanisha timu za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Zanzibar (ZSSF)
  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (SMZ), mama Asha Seif Idd akifuatilia kwa makini mchezo wa netiboli wa tamasha la Pasaka kati ya ZSSF na NSSF uliofanyika kswenye uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar.
 Barke Mohamed wa ZSSF (katika) akichuana na mchezaji wa NSSF Queens
 Mchezaji wa NSSF, Matalena Mhagama akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa ZSSF Queens, Barke Mohamed.
Mashabiki wa timu ya NSSF Queens wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga ZSSF Queens 35-29 katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kweye uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar.
Kikosi cha timu ya NSSF Queens kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na ZSSF Queens. NSSF Queens ilishinda 35-29.

No comments:

Post a Comment