Ndivyo ambavyo Lampard
alivyopiga mpira uliozaa goli la pili na kumpita Julio
Cesar.
Tazama mpira wa Lampard
uliozaa goli safi la pili.
|
Ushindi huo umekuwa ni mwendelezo wa sherehe za maadhimisho ya miaka 150 kuanzishwa kwa chama cha soka cha England FA ambapo England pia rekodi ya kuifunga Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa kombe la dunia.
Wayne Rooney ndiye aliyekuwa wa kwanza kufunga bao uongozi kipindi cha kwanza muda mfupi baada ya penati ya Ronaldinho kuokolewa kistadi na mlinda mlango Joe Hart. Fred aliyeingia kipindi cha pili alifanikiwa kuisawazishia Brazil bao lakini Frank Lampard aliyeingia kipindi cha pili kuandika bao la pili kwa shuti ambalo liligonga mwamba wa kushoto wa mlinda mlango Julio Cesar na kutinga wavuni.
Hata hivyo kikosi cha kilicho katika nafasi ya 6 katika viwango vya ubora vya FIFA kilionekana kikitawala mchezo kwa sehemu kubwa ukilinganisha na Brazil ambao katika viwango vya ubora vya FIFA wako katika nafasi ya 18 huku kiungo Jack Wilshere akitawala vema sehemu ya kiungo.
Uwanja wa Wembley ulikuwa ukisubiri kwa hamu ujio wa nyota wawili wa Brazil Neymar na Ronaldinho, lakini wote walionekana kutokuwa vizuri licha ya kuwa ndio kioo cha Brazil kabla ya mchezo
Frank Lampard akikimbia
kwa furaha baada ya kufunga goli la pili dhidi ya
Brazil.
Ndivyo ambavyo Lampard
alivyopiga mpira uliozaa goli la pili na kumpita Julio
Cesar.
Tazama mpira wa Lampard
uliozaa goli safi la pili
Wayne Rooney akiruka juu akishangilia goli la kwanza
dhidi ya Brazil uwanja wa Wembley.
Julio Cesar akizuia mpira
wa Theo Walcott akiwa karibu na goli baada ya kupokea pasi ya Jack
Wilshere.
Fred wa Brazil akifunga
goli la kusawazisha kipindi cha pili kufuatia makosa ya Gary
Cahill.
David Luiz akiongoza
furaha ya goli la kusawazisha lililofungwa na
Fred.
...Ronaldinho kipiga
penati ambayo haikuzaa goli..
Ronaldinho akitahidi
kupiga mpira kuelekea katika lango la England lakini Joe Hart alikuwa
imara.
Neymar akitengeneza mpira
huku akikabiliwa na upinzani kutoka kwa Tom
Cleverley.
Peter Shilton akimkabidhi
nahodha wa England Steven Gerrard kofia ya kumbukumbu ya dhahabu ikiwa ni ishara
ya heshima kwake baada ya kutimiza michezo 100 ya kuitumikia England mwezi
Novemba katika mchezo dhidi ya Sweden mwaka jana.
Sanamu ya nyota na nahodha
wa zamani wa England Bobby Moore iliyowekwa nje ya uwanja wa England ilikuwa ni
kumbukumbu yake ya miaka 20 tangu kufariki dunia wiki
hii.
Akina dada wakicheza Samba
kuwafurahisha watazamaji zaidi ya elfu 80 waliohudhuria mchezo huo ikiwa ni
ngoma maarufu Marekani ya kusini.
Wacheza shoo wakionyesha shoo ya ngoma ya kibrazil ndani ya uwanja wa Wembley.
Ronaldinho akipewa jezi
ikiwa ni ishara ya utumishi wake wa michezo 100 katika kikosi cha Brazil jezi
hiyo imechorwa namba 100.
Luiz Felipe Scolari
ameiongoza Brazil dhidi ya England akirejea baada ya kupigwa chini mwaka 2006
No comments:
Post a Comment