Marehemu Ismail Mapanga, enzi za
uhai wake.
MPIGA
gitaa la besi wa bendi kongwe ya Msondo Ngoma, Ismail Mapanga, amefariki Dunia
usiku wa kuamkia leo, katika Hospitali ya Temeke, jijini Dar es Salaam na kuacha
pengo kubwa katika bendi hiyo.
Akizungumza na Handeni Kwetu leo
jijini Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo,
Said Kibiriti, alisema taarifa za msiba wa mwanamuziki ni nzito kwao,
huku akitarajiwa kuzikwa leo saa saba mchana.
Kibiriti alisema kifo cha Mapanga
ni pigo kubwa kwa bendi yao, hasa kutokana na mchango wake katika tasnia ya
muziki wa dansi, akiwa na Msondo Ngoma.
Alisema
wamepokea kifo hicho kwa masikitiko makubwa, huku wakiamini kuwa wameumizwa na
msiba huo wa mpiganaji mwenzao, aliyewaacha wapweke.
“Ni
msiba mzito kwetu sisi wa Msondo Ngoma pamoja na wadau wote wa muziki wa dansi
hapa nchini, ukizingatia kwamba marehemu ni kiungo mahiri mno.
“Familia yake imeona azikwe leo
saa saba mchana, huku mwili wake ukiwa nyumbani kwake Tandika, baada ya kufariki
katika Hospitali ya Temeke, alipokuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo,” alisema
Kibiriti.
Hata
hivyo Kibiriti hakutaka kujibu swali la haraka ya mazishi ya mwanamuziki wake,
hali inayoweza kuwanyima fursa ya kuzikwa na wadau na mashabiki wa Msondo kwa
ujumla.
No comments:
Post a Comment