Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, January 20, 2013

MAN CITY YAIKARIBIA MAN UNITED BAADA YA KUVUTWA SHATI JANA

David Silva
 
David Silva alifunga magoli mawili na kuisadia Manchester City, kuilaza Fulham katika uwanja wao wa Etihad na kupunguza idadi ya alama kati yao na vinara wa sasa Manchester United.
Kufuatia ushindi huo, wa magoli mawili kwa bila mabingwa hao watetezi wako alama nne nyuma Manchester United.
United hata hivvyo inangoza kwa kwa tofauti ya alama moja kwani mechi yao dhidi ya Tottenham wametoka sare 1-1.
Katika mechi nyingine, kwa mara ya kwanza washambulizi wa Liverpool Luis Suarez na Daniel Sturridge walicheza pamoja katika mechi moja na kila mmoja wao kufunga bao wakati wa mechi yao dhidi ya Norwich.
Liverpool ilishinda mechi hiyo kwa kuinyuka Norwich magoli matano kwa yai.
Luis Suarez
 
Newcastle nayo ilipoteza alama tatu muhimu katika uwanja wao wa nyumabani pale ilipolimwa magoli mawili kwa moja na Reading.
Adam Le Fondre ambaye aliingia kama mchezaji wa ziada alifunga magoli mawili katika muda wa dakika sita.
Kufuaia kipigo hicho, Newcastle sasa imeshuka hadi nafasi ya 17 na alama 21.
Newcastle hata hivy7o ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa mshambulizi wake Yohan Cabaye.

Jonathan de Guzman alifunga magoli mawili naye Ben Davies akafunga bao moja na kuhakikishia Swansea, alama tatu muhimu za ligi kuu ya premier.
Swansea iliinyeshea Stoke City magoli matatu kwa moja.
Katika matokea mengine West Ham ilitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na QPR nayo Wigan ikafunga magoli 2 - 3 na Sunderland.

No comments:

Post a Comment